AFGHANISTAN-USALAMA

Maafisa 10 wanaohusika na kutegua mabomu wauawa Afghanistan

Mapigano kati ya vikosi vya Taliban na serikali yameongezeka na yameenea katika majimbo 26 kati ya 34 ya Afghanistan tangu Marekani ilipotangaza mwezi wa Aprili kuwa itaondoa wanajeshi wake Septemba 11, maafisa wanasema.
Mapigano kati ya vikosi vya Taliban na serikali yameongezeka na yameenea katika majimbo 26 kati ya 34 ya Afghanistan tangu Marekani ilipotangaza mwezi wa Aprili kuwa itaondoa wanajeshi wake Septemba 11, maafisa wanasema. WAKIL KOHSAR AFP/File

Wapiganaji wa Taliban wamewauwa Waafghanistan 10 wanaofanya kazi kwa shirika kuu linalojishughulisha na kazi ya kutegua mabomu yaliyotegwa ardhini nchini humo, polisi imesema leo Jumatano.

Matangazo ya kibiashara

Wapiganaji wa Kiisilamu Jumanne jioni walishambulia kambi ambayo ilikuwa ikitumiwa kama hifadhi kwa wafanyakazi hawa, katika mkoa wa Baghlan, kaskazini mwa Afghanistan, eneo lililokabiliwa na mapigano makali katika wiki za hivi karibuni.

"Taliban waliwachukua na kuwapeleka katika chumba kimoja  na kuwafyatulia risasi," ameema msemaji wa polisi wa mkoa huo Jawed Basharat, ambaye pia aliripoti majeruhi 14.

Jawed Basharat amebaini kwamba wahanga walikuwa wakifanya kazi katika shirika la Halo Trust, shirika kuu linalojihusisha katika juhudi za kuondoa mabomu na vifaa vingine vya kulipuka vinavyoripotiwa nchini kote Afghanistan baada ya miongo kadhaa ya mizozo.

Mapigano kati ya vikosi vya Taliban na serikali yameongezeka na yameenea katika majimbo 26 kati ya 34 ya Afghanistan tangu Marekani ilipotangaza mwezi wa Aprili kuwa itaondoa wanajeshi wake Septemba 11, maafisa wanasema.