MAREKANI-USHIRIKIANO

Marekani yawaondolea vikwazo maafisa wa zamani wa Iran

Uamuzi huu wa Ofisi ya Udhibiti wa Mali za Kigeni ya Wizara ya Fedha ya Marekani (OFAC) hauhusiani na juhudi zinazoendelea za kuirejesha Marekani na Iran chini ya makubaliano ya nyuklia ya Iran ya 2015, amesema afisa mmoja wa Marekani, ambaye hakutaka jina lake litajwe.
Wizara ya Fedha imesema OFAC na Wizara ya Mambo ya Nje wameondoa "vikwazo dhidi ya maafisa watatu wa zamani wa serikali ya Iran na kampuni mbili zilizohusika hapo hapo zamani katika kuuza, kununua, kusafirisha bidhaa ya mafuta kutoka Iran.
Msemaji wa Wizara ya Fedha amebaini kwamba wawakilishi hao watatu wa Iran walionyesha kwamba hawashikilii tena wadhifa wowote "katika vyombo vinavyohusiana na serikali" huko Tehran na kuongeza kuwa kwa hakuna sababu zaidi ya kuendeleza vikwazo.
Uamuzi huu wa Ofisi ya Udhibiti wa Mali za Kigeni ya Wizara ya Fedha ya Marekani (OFAC) hauhusiani na juhudi zinazoendelea za kuirejesha Marekani na Iran chini ya makubaliano ya nyuklia ya Iran ya 2015, amesema afisa mmoja wa Marekani, ambaye hakutaka jina lake litajwe. Wizara ya Fedha imesema OFAC na Wizara ya Mambo ya Nje wameondoa "vikwazo dhidi ya maafisa watatu wa zamani wa serikali ya Iran na kampuni mbili zilizohusika hapo hapo zamani katika kuuza, kununua, kusafirisha bidhaa ya mafuta kutoka Iran. Msemaji wa Wizara ya Fedha amebaini kwamba wawakilishi hao watatu wa Iran walionyesha kwamba hawashikilii tena wadhifa wowote "katika vyombo vinavyohusiana na serikali" huko Tehran na kuongeza kuwa kwa hakuna sababu zaidi ya kuendeleza vikwazo. © REUTERS - TOM BRENNER

Marekani imetangaza kwamba imeondoa vikwazo dhidi ya maafisa watatu wa zamani wa Iran na kampuni mbili za Iran zilizohusika katika biashara ya bidhaa ya petroli hapo zamani, hatua iliyoelezwa na afisa wa Marekani kama ya kawaida lakini ambayo inaweza kuonyesha nia ya Washington ya kulegeza vikwazo dhidi ya Tehran ikiwa itahitajika.

Matangazo ya kibiashara