YEMEN-USALAMA

Yemen: Nane waangamaia katika shambulio linalodaiwa kutekelezwa na Wahouthiouthi

Mapema mwezi huu, watu wasiopungua 17 walifariki dunia katika mlipuko uliotokea karibu na kituo cha mafuta huko Marib, mlipuko ambao serikali ilisema ulisababishwa na kombora lililofyatuliwa na waasi wa Houthis.
Mapema mwezi huu, watu wasiopungua 17 walifariki dunia katika mlipuko uliotokea karibu na kituo cha mafuta huko Marib, mlipuko ambao serikali ilisema ulisababishwa na kombora lililofyatuliwa na waasi wa Houthis. - AFP

Angalau watu wanane waliuawa katika milipuko katika mji wa Marib wa Yemen siku ya Alhamisi, mamlaka wamesema, wakati serikali inayotambuliwa kimataifa ikilaani shambulio la waasi wa Kishia wa Houthi wakijaribu kuteka eneo hilo lenye mafuta ya petroli.

Matangazo ya kibiashara

Waziri wa Habari amesema kupitia Twitter kwamba waasi walirusha makombora mawili ya masafa marefu ambayo yalilenga msikiti, jengo la biadhara na kituo cha mahabusu cha wanawake.

Muanmar al-Iryani amesema ripoti ya awali inabaini vifo vya watu wanane, ikiwa ni pamoja na wanawake, na karibuwatu wengine thelathini walijeruhiwa.

Msemaji wa jeshi la Yemen, akizungumza kwenye runinga, amesema makombora mawili yalirushwa, moja lilianguka katika eneo la makazi na lingine sokoni. Ndege mbili zisizo kuwa na rubani pia zilitumiwa katikashambulio hilo.

Hii ni "milipuko mikubwa iliyosikika huko Marib katika miaka minne," mkazi wa jiji hilo Abdoulsalam Ghaleb ameliambia shirika la habari la REUTERS.

Mapema mwezi huu, watu wasiopungua 17 walifariki dunia katika mlipuko uliotokea karibu na kituo cha mafuta huko Marib, mlipuko ambao serikali ilisema ulisababishwa na kombora lililofyatuliwa na waasi wa Houthis.

Muungano unaoongozwa na Saudi Arabia, ambao umekuwa ukiingilia kati kijeshi nchini Yemen dhidi ya Wahouthi tangu mwaka 2015, ulitangaza siku ya Alhamisi kuwa uliharibu ndege isiyo kuwa na rubani iliyorushwa na waasi kuelekea kusini mwa Saudi Arabia.