Palestina yautaka umoja wa mataifa kuishutumu Israeli kwa ukiukaji wa haki za watoto

Waziri mkuu wa Palestina Mohammad Shtayyeh akiwa mbele ya waandishi wa habari 2018
Waziri mkuu wa Palestina Mohammad Shtayyeh akiwa mbele ya waandishi wa habari 2018 © Ikulu ya Palestina

Waziri mkuu wa Palestina, Mohammad Shtayyeh, ametoa wito kwa katibu mkuu wa umoja wa Mataifa, kuirodhesha nchi ya Israel kama moja ya mataifa ambayo yanakiuka haki za watoto duniani.

Matangazo ya kibiashara

Shtayyeh, ametoa matamshi haya wakati wa kikao cha baraza la mawaziri, ambapo ameituhumu nchi ya Israel kwa kuendelea kukiuka haki za watoto wa Kipalestina, huku akiinyooshea kidole kwa kujaribu kuwapa chanjo za Covid 19 ambazo zimeisha muda wake.

Waziri mkuu wa mamlaka ya Palestina Mohammad Shtayyeh, amemtuhumu waziri mkuu aliyeondoka madarahani hivi karibuni Benjamin Netanyahu kwa kuchochea hatua hiyo, ambapo hata hivyo mtuhumiwa hajatoa tamko lolote kuhusu madai hayo.

Kikao cha hivi leo jumatatu cha umoja wa mataifa kimelitaka shirika linalowashughulikia watoto duniani la Unicef, kufanya uchunguzi kuhusu tuhuma hizo kabla ya kuchukua hatua hiyo, ambayo hata hivyo imeonekana kutoungwa mkono na washiriki