LIBANON-SIASA

Hariri awasilisha majina ya wajumbe wa serikali yake kwa Rais Aoun

Waziri Mkuu Mteule wa Lebanon Saad al-Hariri amewasili ikulu kukutana na Rais wa Lebanon Michel Aoun huko Baabda, Lebanon Julai 14, 2021.
Waziri Mkuu Mteule wa Lebanon Saad al-Hariri amewasili ikulu kukutana na Rais wa Lebanon Michel Aoun huko Baabda, Lebanon Julai 14, 2021. AFP

Waziri Mkuu mteule wa Lebanon, Saad Hariri ametangaza Jumatano wiki hii kuwa amempa Rais Michel Aoun orodha ya mawaziri wanaowezekana kuunda serikali na anatarajia kupata jibu Alhamisi kumaliza msukosuko wa kisiasa ambao umedumu kwa zaidi ya miezi tisa.

Matangazo ya kibiashara

"Huu ni wakati wa ukweli," amesema Saad Hariri, ambaye hapo awali alikuwa mkuu wa serikali ya Lebanon.

Lebanon imekosa serikali tangu timu ya mwisho ya uongozi hatimaye iliondoka wiki chache baada ya mlipuko wa Agosti 4, 2020 ambao uliua mamia na kuharibu mji mkuu wa nchi hiyo, Beirut.

Mkwamo wa kisiasa umeongeza mgogoro wa kifedha nchini, ambao Benki ya Dunia imeuita unyogovu mbaya zaidi katika historia ya kisasa.

"Kwa maoni yangu, serikali hii ina uwezo wa kuokoa nchi na kuzuia kutumbukia katika mdororo wa kiuchumi," amesema Saad Hariri, aliyeteuliwa mwezi Oktoba uliyopita kuunda serikali, lakini ambaye amepata shida kubwa katika kuunda baraza la mawaziri la umoja wa kitaifa kutokana na kiwango cha mgogoro wa kisiasa, kiuchumi na kijamii.

Ufaransa imekuwa ikidai kwa miezi kadhaa kuundwa kwa serikali mpya na utekelezaji wa mageuzi kama sharti la kuruhusiwa kupewa msaada wa mabilioni ya dola.