AFGHANISTAN

Afghanistan: Mapigano ya udhibiti wa eneo la mpakani na Pakistan yazuka

Umati wa watu wakipeperusha bendera ya Taliban huko Chaman, mpakani mwa Afghanistan na Pakistan.
Umati wa watu wakipeperusha bendera ya Taliban huko Chaman, mpakani mwa Afghanistan na Pakistan. AFP - ASGHAR ACHAKZAI

Vikosi vya serikali ya Afghanistan vimepata udhibiti wa eneo muhimu la mpakani kati ya Afghanistan na Pakistan lillokuwa limedhibitiwa kwa muda mfupi na Taliban, afisa mwandamizi wa serikali huko Kabul amesema leoAlhamisi, madai yaliyokanushwa na waasi wa Kiisilamu.

Matangazo ya kibiashara

Siku ya Jumatano Taliban waliteka eneo la Spin Boldak-Chaman, eneo la pili muhimu zaidi kati ya Afghanistan na Pakistan, ambalo ni chanzo muhimu cha mapato kwa serikali ya Afghanistan.

Lakini vikosi vya Afghanistan vilipata tena udhibiti wa soko kuu la mji huo wa mpakani masaa kadhaa baadaye, ikiwa ni pamoja na jengo la idara ya forodha na vifaa vingine kadhaa vya serikali, amesema afisa mwandamizi wa serikali aliyeko katika mkoa wa Kandahar, ambapo eneo la Spin Boldak linapatikana.

Vikosi vya serikali, ambavyo hapo awali viliamuwa kuondoka ili kupunguza majeruhi, vimekuwa vikiwasaka wapiganaji wa kundi hilo, afisa huyo ameongeza.