LEBANON-SIASA

Lebanon: Waziri Mkuu mteule Saad Hariri ajiuzulu

Waziri Mkuu mteule wa Lebanon Saad al-Hariri wakati akitangaza kuwa anaajiuzulu kwenye nafasi yake baada ya kukutana na rais wa Lebanon Michel Aoun katika ikulu ya rais Baabda, Lebanon Julai 15, 2021.
Waziri Mkuu mteule wa Lebanon Saad al-Hariri wakati akitangaza kuwa anaajiuzulu kwenye nafasi yake baada ya kukutana na rais wa Lebanon Michel Aoun katika ikulu ya rais Baabda, Lebanon Julai 15, 2021. REUTERS - DALATI NOHRA

Waziri Mkuu mteule wa Lebanon Saad Hariri ametangaza leo Alhamisi kwamba anajiuzulu kwenye nafasi yake karibu miezi tisa baada ya kuteuliwa.

Matangazo ya kibiashara

Uamuzi huu unakuja wakati Lebanon inakabiliwa na mzozo mbaya zaidi wa kijamii na kiuchumi katika historia yake.

Saad Hariri aliteuliwa kuwa Waziri Mkuu mwezi Oktoba 2020 na alikuwa akiunda timu inayopaswa kuzindua mageuzi muhimu ili kuwezesha kupata hasa misaada muhimu ya kimataifa . Amewaambia waandishi wa habari leo Alhamisi kwamba alikuwa amekutana na rais Michel Aoun ambaye alikuwa ametaka marekebisho kwenye orodha ya wajumbe wa serikali, mabadiliko ambayo alikuwa amepinga.

"Ni wazi kwamba msimamo (wa Michel Aoun) haujabadilika juu ya suala hili na kwamba hatutaweza kukubaliana," amesema. "Nilimpa muda zaidi wa kufikiria na akasema" Hatuwezi kufikia makubaliano ". Ndio maana nimeomba radhi kwa kutoweza kuunda serikali, Mungu asaidie nchi hii. "

Michel Aoun na Saad Hariri wameonyesha mara kwa mara kutokubaliana kwao katika miezi ya hivi karibuni, hasa wakati wa waliposhambuliana hadharani mwezi Machi baada ya mkutano mwingine ambao ulikumbwa na tuhuma kutoka pande mbili.

Saad Hariri alimkosoa rais kwa kukwamisha uundaji wa serikali kwa kusisitiza juu ya "wachache wanaozuia" katika baraza jipya la mawaziri na kwa kutaka kulazimisha kugawana madaraka. Ikulu ya rais ilikanusha dalili yoyote ya "kuzuia wachache" na kuelezea "kushangaa" kwa "matamshi" ya Saad Hariri.

Saad Hariri, ambaye aliteuliwa mara tatu kuwa Waziri Mkuu Oktoba 22, 2020, mwaka mmoja baada ya kuachia ngazi chini ya shinikizo la maandamano. Serikali ya sasa, inayosimamia maswala ya sasa, ilikuwa imejiuzulu baada ya mlipuko mbaya katika bandari ya Beirut ambao ulisababisha vifo vya watu zaidi ya 200 na maelfu kujeruhiwa, Agosti 4, 2020.