IRAN-USALAMA

Maandamano yazuka juu ya uhaba wa maji Iran

Mnamo mwezi Mei, Waziri wa Nishati wa Iran Reza Ardakanian alionya juu ya uhaba wa maji katika msimu wa joto, akisema mwaka huu ni "moja ya miaka iliyokumbwa zaidi ukame tangu miaka 50 iliyopita."
Mnamo mwezi Mei, Waziri wa Nishati wa Iran Reza Ardakanian alionya juu ya uhaba wa maji katika msimu wa joto, akisema mwaka huu ni "moja ya miaka iliyokumbwa zaidi ukame tangu miaka 50 iliyopita." AFP - ATTA KENARE

Maandamano yamezuka usiku wa kuamkia Ijumaa wiki hii kufuatia uhaba mkubwa wa maji, Kusini magharibi mwa Iran, eneo lenye utajiri wa mafuta, kulingana na vyombo vya habari vya Iran na video zilizorushwa hewani kwenye mitandao ya kijamii siku ya Ijumaa wakati nchi hiyo inakabiliwa na ukame  mbaya zaidi tangu miaka 50 iliyopita.

Matangazo ya kibiashara

Video zinaonyesha waandamanaji wakichoma matairi kuzuia barabara na vikosi vya usalama vikijaribu kutawanya umati wa watu wakati milio ya risasi ikisikika, kulingana na shirika la habari la REUTERS ambalo limebaini kwamba halikuweza kuchunguza kwa njia iliyo huru uhalisia wa video hizi.

"Televisheni ya umma inapaswa kuripoti kile tunachosema na kuonyesha picha ya nyati ambao waliangamia kwa kukosa maji," amesema mmoja wa waandamanaji katika video iliyotolewa na tovuti ya habari ya mkoa wa Asrejonoob.

Mnamo mwezi Mei, Waziri wa Nishati wa Iran Reza Ardakanian alionya juu ya uhaba wa maji katika msimu wa joto, akisema mwaka huu ni "moja ya miaka iliyokumbwa zaidi ukame tangu miaka 50 iliyopita."

Uhaba wa maji ulisababisha kukata kwa umeme na kufuatiwa na maandamano katika miji kadhaa wiki iliyopita. Wengine walionyesha hasira zao kwa Kiongozi Mkuu Ayatollah Ali Khamenei, wakiimba na kutoa maneneo ya kashfa dhidi ya kiongozi huyo.

Uchumi wa Iran umeanguka kutokana na vikwazo vya Marekani na janga la COVID-19, na nchi hiyo imeathirika zaidi na virusi vya Corona katika ukanda wa Mashariki ya Kati.