LEBANON-SIASA

Ufaransa yataka uteuzi wa Waziri Mkuu mpya nchini Lebanon

wAZIRI mKUU mTEULE Saad HarirI amejiuzulu baada ya kushauriana na rais Michel Aoun.
wAZIRI mKUU mTEULE Saad HarirI amejiuzulu baada ya kushauriana na rais Michel Aoun. ANWAR AMRO AFP/Archivos

Ufaransa inasema imepokea uamuzi wa Waziri Mkuu mteule wa Lebanon Saad Hariri kujiuzulu baada ya kushindwa kuunda serikali kwa muda miezi minane sasa na kutaka uteuzi wa mrithi wake bila kuchelewa.

Matangazo ya kibiashara

Katika taarifa kwa vyombo vya habari, Wizara ya Mambo ya nje ya Ufaransa imesisiiza juu ya "dharura kabisa ya kuondokana na hali hii iliyopangwa na isiyokubalika" nchini Lebanon.

Ameongeza kuwa mkutano mpya wa kimataifa kuunga mkono raia wa Lebanon utafanyika Agosti 4.

Hariri amesema amefikia uamuzi huo baada ya kushauriana na rais Michel Aoun.