SAUDI ARABIA

Mahujaji waanza ibada ya Hija Makka kwa idadi ndogo kwa sababu ya Covid

Mwaka huu wa 2021, mahujaji wameruhusiwa kushiriki katika ibada ya Hija huko Makka kwa idadi ndogo, mbali na umati ambao kawaida huonekana wakati huu katika Jiji hilo Takatifu. Mwaka huu, ni wakaazi tu waliopewa chanjo kamili dhidi ya Covid-19 ndio wameruhusiwa, sawa na karibu watu 60,000.
Mwaka huu wa 2021, mahujaji wameruhusiwa kushiriki katika ibada ya Hija huko Makka kwa idadi ndogo, mbali na umati ambao kawaida huonekana wakati huu katika Jiji hilo Takatifu. Mwaka huu, ni wakaazi tu waliopewa chanjo kamili dhidi ya Covid-19 ndio wameruhusiwa, sawa na karibu watu 60,000. © AFP - STR

Mahujaji wameanza kuwasili Makka, mji mtakatifu wa Uislam nchini Saudi Arabia, kushiriki kuanzia Jumamosi hii katika Hija kuu ya kila mwaka, Lakini mahujaji wameonekana wakishiriki ibada hiyo kwa miaka miwili mfululizo kwa idadi ndogo kwa sababu ya mgogoro wa kiafya unaosababishwa na Covid.

Matangazo ya kibiashara

Mwaka huu, Wasaudi na wageni 60,000 tu wanaoishi nchini Saudi Arabia na waliopewa chanjo ndio wameruhusiwa kushiriki ibada hiyo kuu ya Hija. Mwaka wa 2020, mahujaji elfu kumi tu waliweza kushiriki ibada hiyo.

Mwaka 2019, kabla ya kuzuka kwa janga hilo hatari, mahujaji Milioni 2.5 ambao walikuja kutoka ulimwenguni kote walikuja Makka kushiriki katika moja ya ibada kubwa ya kidini kwa Waislamu.

Mahujaji hao watagawanywa katika makundi ya watu 20 ili "kupunguza kuenea kwa virusi" iwapo yeyote kati yao atakuwa na maambukizi, Mohammed al-Bijaoui, mmoja wa maafisa wa Saudi arabia amesema kwenye runinga.

Mahujaji pia hawataweza kugusa Kaaba, muundo wa ujazo unaopatikana katika mji wa Makka, ambao Waislamu kote ulimwenguni wanaelekea wakati wanaposwali.