SYRIA-SIASA

Syria: Assad atawazwa, raia sita wauawa kwa mashambulizi

Wasyria wanakishikilia bendera ya nchi na picha ya Bashar al-Assad Mei 27, 2021 huko Damascus, siku moja baada ya uchaguzi wa rais ambao alitngazwa mshindi
Wasyria wanakishikilia bendera ya nchi na picha ya Bashar al-Assad Mei 27, 2021 huko Damascus, siku moja baada ya uchaguzi wa rais ambao alitngazwa mshindi LOUAI BESHARA AFP

Rais wa Syria Bashar al-Assad ameapishwa Jumamosi kwa muhula wa nne katika hafla iliyofanyika katika ikulu ya rais huko Damascus baada ya kushinda 95.1% ya kura katika uchaguzi wa urais wa Mei 26, uliyokosolewa na nchi za Magharibi na upinzani nchini Syria

Matangazo ya kibiashara

Bwana Assad ambaye yuko madarakani tangu mwaka 2000, ameapishwa akishika Katiba na Qoran mbele ya wageni zaidi ya 600, wakiwemo mawaziri, wafanyabiashara, wasomi na waandishi wa habari, kulingana na waandaaji wa hafla hiyo, katika nchi iliyoharibiwa na vita vilivyodumu zaidi ya miaka kumi ambavyo viliua watu karibu nusu milioni.

Wakati huo huo mashambulizi ya anga ya vikosi vya serikali katika mkoa wa Idlib kaskazini magharibi mwa Syria, yameua raia sita, wakiwemo watoto watatu.

Uchaguzi wa urais "ulithibitisha nguvu ya utawala halali uliopewa na raia kwa taifa hili na kudharau taarifa za maafisa kutoka nchi za Magharibi juu ya uhalali wa serikali, Katiba na nchi," Bwana Assad aamesema katika ufunguzi wa hotuba yake ya kuapishwa.

Mwezi Mei Washington na madola kadhaa ya Ulaya yalilaani uchaguzi huo na kusema "haukuwa huru na wa haki", wakati upinzani ulishutumu "udanganyifu mkuwa" wa uchaguzikatika nchi hiyo iliyokumbwa na mgogoro mkubwa wa kiuchumi na kifedha.

Syria inakabiliwa na kushuka kwa thamani ya sarafu yake, mfumuko wa bei unaopungua na kiwango cha umasikini kinachoathiri zaidi ya asilimia 80 ya wakaazi wake, kulingana na Umoja wa Mataifa.