ISRAELI

Safari za ndege kutoka Tel Aviv kwenda Marrakech zaanza

Baada ya Falme za Kiarabu, Bahrain na Sudan, serikali ya Kiyahudi ilifungua ukurasa mpya wa kidiplomasia mwezi wa Desemba 2020  kwa kurejesha uhusiano na nchi za Kiarabu.
Baada ya Falme za Kiarabu, Bahrain na Sudan, serikali ya Kiyahudi ilifungua ukurasa mpya wa kidiplomasia mwezi wa Desemba 2020 kwa kurejesha uhusiano na nchi za Kiarabu. GIL COHEN-MAGEN AFP/File

Mashirika mawili ya ndege ya Israeli yamezindua Jumaili hii safari za moja kwa moja za kibiashara kati ya Tel Aviv na Marrakech kama sehemu ya kurejesha uhusiano kati ya Israeli na Morocco zilizokubaliana chini ya mwavuli wa Marekani mwaka jana.

Matangazo ya kibiashara

Ndege ya shirika la Israeli la EL AL Israel Airlines, chapa 553 iliondoka saa 11:35 mchana (sawa na saa 8:35 saa za kimataifa) kwa safari ya saa sita. Ndegeya shirika la ndege la  Israeli ya Israir pia iliruka saa 8:15 asubuhi (sawa na saa 5:15 asubuhi saa za kimataifa) kuelekea Morocco.

Shirika la tatu la ndege la Israeli, Arkia, pamoja na Royal Air Maroc pia zinatarajia kuanza safari kati ya Tel Aviv na Marrakech mwezi ujao.

"Safari hizi zitasaidia kukuza utalii, biashara na ushirikiano wa kiuchumi kati ya nchi hizi mbili," Waziri wa Utalii wa Israeli Yoel Razvozov amesema.

EL AL imepanga kufanya safari hadi tano kwa wiki kwenda Morocco, ambayo iliipa hifadhi mojawapo ya jamii kubwa zaidi ya Kiyahudi huko Afrika Kaskazini na Mashariki ya Kati kwa karne nyingi hadi taifa la Israeli lilipoanzishwa mwaka wa 1948. Wayahudi 3,000 bado wanaishi Morocco na mamia ya maelfu ya Waisraeli wanadai kuwa ni wenye asili ya Morocco.

Baada ya Falme za Kiarabu, Bahrain na Sudan, serikali ya Kiyahudi ilifungua ukurasa mpya wa kidiplomasia mwezi wa Desemba 2020  kwa kurejesha uhusiano na nchi za Kiarabu.