MAREKANI-USHIRIKIANO

Marekani kusitisha operesheni zake Iraq mwishoni mwa mwaka huu

Kwa pamoja vita vya Afghanistan na Iraq vimeligharibu kwa kiwango kikubwa jeshi la Marekani na kulizuia kuondoka katika maeneo hayo na hasa baada ya kuongezea kwa mvutano na China, ambo Biden mwenyewe amenukuliwa akisema kuwa ni changamoto kubwa na ya muda mrefu.
Kwa pamoja vita vya Afghanistan na Iraq vimeligharibu kwa kiwango kikubwa jeshi la Marekani na kulizuia kuondoka katika maeneo hayo na hasa baada ya kuongezea kwa mvutano na China, ambo Biden mwenyewe amenukuliwa akisema kuwa ni changamoto kubwa na ya muda mrefu. REUTERS

Rais Joe Biden wa Marekani ametangaza kwamba Marekani itaondoa vikosi vyake nchini Iraq, baada ya kusitisha operesheni zake za kijeshi mwishoni mwa mwaka huu.

Matangazo ya kibiashara

Rais wa Marekani ametoa tangazo hilo baada ya uamuzi wake wa kuliondoa jeshi la Marekani kwa ukamilifu nchini Afghanistan, ikiwa ni baada ya Marekani kuanzisha mashambulizi ya kujibu mapigo ya mashambulizi ya kigaidi ya New York ya Septemba 11,2001.

Tangazo hilo lilikuja baada ya Joe Biden kufanya mazungumzo na Waziri Mkuu wa Iraq Mustafa al-Kadhimi katika Ikulu ya White House.

Pamoja na kwamba bado kitisho cha kundi la Dola la Kiislamu kipo na ushawishi wenye nguvu wa Iran kwa Iraq, lakini Biden amesisitiza kwamba serikali yake itasalia jukumu la kuimarisha ushirikiano wa kiusalama.

Tunauga mkono uimarishaji wa demokrasia nchini Iraq, na tunafuatilia hakikisha kuwa Uchaguzi unafanyika mwezi Oktoba. Tunaendelea kuwa na nia ya kushirikiana katika masuala ya usalama na kupambana na ISIS. Ni muhimu kuwa na ukanda ulio thabiti na ushirikiano wetu dhidi ya gaidi utaendelea, na haya ndio mambo ambayo tutayajadili. 

Vyama vya kisiasa vinavyoegemea upande wa Iran vimetaka kuondolewa kwa vikosi vyote kutoka kwa muungano wa kimataifa unaoongozwa na Marekani dhidi ya IS, licha ya tishio linaloendelea kutolewa na kundi hilo la kijihadi la Sunni.

Kwa pamoja vita vya Afghanistan na Iraq vimeligharibu kwa kiwango kikubwa jeshi la Marekani na kulizuia kuondoka katika maeneo hayo na hasa baada ya kuongezea kwa mvutano na China, ambo Biden mwenyewe amenukuliwa akisema kuwa ni changamoto kubwa na ya muda mrefu.