IRAN

Iran: Ayatollah Ali Khamenei azivalia njuga nchi za Magharibi

Picha iliyotolewa na ofisi ya Kiongozi Mkuu wa Iran Ayatollah Ali Khamenei  Julai 28, 2021, inamuonyesha wakati wa mkutano na rais na baraza lake la mawaziri katika mji mkuu Tehran.
Picha iliyotolewa na ofisi ya Kiongozi Mkuu wa Iran Ayatollah Ali Khamenei Julai 28, 2021, inamuonyesha wakati wa mkutano na rais na baraza lake la mawaziri katika mji mkuu Tehran. AFP - -

Kiongozi Mkuu wa Iran Ayatollah Ali Khamenei amemkosoa waziwazi rais Hassan Rouhani, akisema uzoefu wa serikali yake umethibitisha kwamba nchi za Magharibi na Merika haziwezi kuaminika.

Matangazo ya kibiashara

Ali Khamenei, ambaye alikuwa akiwawapokea wajumbe wa serikali ya rais Rouhani kwa mara ya mwisho, ameonyesha msimamo wako na kusema wazi wazi. “Uzoefu wa serikali yenu umeonyesha kuwa kuamini nchi za Magharibi ni jambo lisilokuwa na maana. Hawatusaidii na jambo walillotaka kufanya walilifanya, ”Ayatollah Khamenei amesema.

Hassan Rohani na serikali yake bado wanahudumu kwa siku chache. Rais ajaye, Ebrahim Raïssi anatarajia kuingia madarakani Agosti 5, sawa na wiki moja inayosalia.

Kiongozi wa juu kabisa nchini Iran pia ameikosoa Marekani, akisema haikutaka kuondoa vikwazo vilivyowekwa dhidi ya Iran tangu mwaka 2018 na Rais wa zamani Donald Trump.

"Kupitia kauli zao, wanasema wanaondoa vikwazo. Hawakutekeleza hilo na hawatatekeleza. Wanaweka masharti, ”amesema Ali Khamenei, na kuongeza kuwa Wamarekani wanataka kujumuisha mpango wa makombora ya masafa marefu na sera ya kikanda katika mazungumzo yajayo.

Serikali ya Rouhani ilikuwa kwenye mazungumzo na nchi zenye nguvu mjini Vienna tangu mwezi Aprili kuhusu kuirudisha tena Marekani katika makubaliano ya Nyuklia ya mwaka 2015, lakini inaonesha hakuna uwezekano wa kufikiwa kwa makubaliano hayo hivi sasa.