AFGHANISTAN-USALAMA

Makao Makuu ya UN yashambulia nchini Afghanistan, mtu mmoja auawa

Gari lililoharibiwa na moja ya roketi tatu zilizorushwa karibu na ikulu ya rais huko Kabul, Julai 20, 2021.
Gari lililoharibiwa na moja ya roketi tatu zilizorushwa karibu na ikulu ya rais huko Kabul, Julai 20, 2021. AP - Rahmat Gul

Makao Makuu ya Umoja wa Mataifa huko Herat, magharibi mwa Afghanistan, yamelengwa na shambulio Ijumaa wiki hii ambalo lilimeuua afisa mmoja wa polisi wa Afghanistan na kujeruhi wengine kadhaa, Umoja wa Mataifa umetangaza, huku ukinyooshea kidole cha lawama waasi wanaopinga serikali ya nchi hiyo.

Matangazo ya kibiashara

Shambulio hili linakuja saa chache baada ya Taliban kuingia Herat, mji mkuu wa mkoa wenye jina kama hilo.

Mapigano kati ya waasi na vikosi vya serikali ya Afghanistan yameftokea karibu na makao makuu ya Ujumbe wa Umoja wa Mataifa nchini Afghanistan (UNAMA).

Umoja wa Mataifa umesema katika taarifa yake kuwa unawasiliana na pande zinazohusika na kujaribu kutoa mwanga juu ya tukio hilo.

Haijulikani bado ni nani aliyeshambulia makao makuu ya Umoja wa Mataifa. UNAMA imesema shambulio hilo lilitokea mbele ya mlango wa eneo linalotambuliwa kuwa ni la Umoja wa Mataifa.

Mapigano yaendelea katika maeneo mengine Afghanistan

"Shambulio hili kwa Umoja wa Mataifa ni la kusikitisha na tunalaani vikali kitendo hiki," amesema Deborah Lyons, mwakilishi maalum wa katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa nchini Afghanistan.

Hakuna mfanyakazi wa Umoja wa Mataifa aliyejeruhiwa katika shambulio hilo, kulingana na UNAMA.

.Hata hivyo, kunaripotiwa mapigano makali kwa siku mbili mfululizo kati ya Taliban na vikosi vya usalama vya Afghanistan huko Lashkar Gah, mji mkuu wa mkoa wa Helmand, kusini mwa Afghanistan.