ISRAEL

Shambulio la Meli ya mafuta Oman: Israeli kuwasilisha kesi kwa Umoja wa Mataifa

Mercer Street ilishambulia Alhamisi Julai 29, 2021, hapa ilikuwa mwaka 2016 karibu na Cape Town nchini Afrika Kusini.
Mercer Street ilishambulia Alhamisi Julai 29, 2021, hapa ilikuwa mwaka 2016 karibu na Cape Town nchini Afrika Kusini. © Johan Victor/AP

Israeli imetaka hatua ya kimataifa ichukuliwe dhidi ya Iran baada ya shambulio baya katika Bahari ya Arabia (Oman) dhidi ya meli ya mafuta inayosimamiwa  na bilionea wa Israeli, ikiituhumu Tehran kwa "ugaidi".

Matangazo ya kibiashara

Mmiliki wa meli Zodiac Maritime, kampuni ya Eyal Ofer kutoka Israel, imetangaza Ijumaa wiki hii "vifo vya wafanyiakazi wawili: raia wa Romania na raia wa Uingereza" wakati wa tukio hilo katika meli ya M / T Mercer Street, iliyotokea Alhamisi wiki hii saa 12 jioni, kulingana na tovuti ya UKMTO kampuni inayojihusisha na shughuli za baharini.

Jeshi la Marekani limesema limeitikia wito wa dhiki, na kuongeza kuwa vikosi vimezuru eneo hilo na kuona ushahidi wa shambulio. Matokeo ya kwanza "yanaonyesha wazi" shambulio lililoendeshwa na ndee isiyo kuwa na rubani.

Hakuna kundi lililodai kuhusika na shambulio hilo lakini kampuni ya Dryad Global, iliyobobea katika usalama wa baharini, imebaini juu ya "ulipizaji kisasi katika vita vikali kati ya nchi hizi mili adui", ikimaanisha Iran na Israeli.