Pata taarifa kuu
MICHEZO 2015

Ulimwengu wa michezo mwaka 2015

Mpiga picha akisubiri nje ya makao makuu ya FIFA, Oktoba 20, 2015, Zurich.
Mpiga picha akisubiri nje ya makao makuu ya FIFA, Oktoba 20, 2015, Zurich. AFP PHOTO / FABRICE COFFRINI
Ujumbe kutoka: RFI
6 Dakika

Kati ya mwezi Januari na mwezi Februari michuano ya soka ya kuwania ubingwa wa Afrika ilichezwa nchini Equaitorial Guinea.

Matangazo ya kibiashara

Timu ya taifa ya Ivory Coast iliibuka mabingwa baada ya kuishinda Ghana mabao 9 kwa 8 kupitia mikwaju ya penalti baada ya timu hizo kutoka sare ya kutofungana katika muda wa kawaida na ule wa ziada.

Fainali za mwaka huu ziliingia utata kidogo baada ya Morroco kujiondoa kuwa wenyeji kwa hofu ya ugonjwa hatari wa Ebola ambao ulikuwa unasababisha mauaji ya watu nchini Guinea, Liberia, na Sireleon.

Tukisalia barani Afrika na katika mchezo wa soka, klabu ya Es Setif ya Algeria iliibuka mabingwa wa taji la Super Cup barani Afrika baada ya kuishinda Al-Ahly ya Misri mabao 6 kwa 5 kupitia mikwaju ya penalti.

Fainali hii ilipigwa mwezi Machi na hufanyika kila mwaka, kumkutanisha bingwa wa taji la klabu bingwa na Shirikisho barani Afrika.

Fainali ya mwaka ujao itakuwa kati ya TP Mazembe mabingwa wa mwaka 2015 kutoka Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo na Etoile du Sahel ya Tunisia, mabingwa wa taji la Shirikisho na mchuano huo utapigwa mwishoni mwa mwezi Februari mjini Lubumbashi.

Riadhaa

Makala ya 41 ya mashindano ya nyika ya dunia au Cross Cross Country yalifanyika mwishoni mwa mwezi Machi nchini China.

Wanaridha zaidi ya mia nne kutoka mataifa 51 walishiriki katika mbio za Kilimota 12, 8 na 6.

Ushindani mkali ulikuwa kati ya wanaridha wa Kenya na Ethiopia.

Wanariadha wa Ethiopia walishika nafasi ya kwanza kwa kupata medali 11, wakifuatiwa na Kenya iliyopata medali 9 na Bahrain kumaliza ya tatu kwa medali 2.

Mashindano yajayo ya mwaka 2017 yatafanyika jijini Kampala nchini Uganda.

Lakini mashindano ya riadha yatakayokumbukwa sana ni yale ya dunia yaliyofanyika jijini Beijing China mwezi wa Agosti.

Wanariadha zaidi ya elfu moja kutoka mataifa 205 walishiriki na nchi ya Kenya ikaweka historia kwa kushinda medali zaidi ya kuwa ya kwanza duniani.

Wanariadha wa Kenya walipata medali saba za dhahabu, sita za fedha, na tatu za shaba na kwa jumla kupata medali 16, ikifuatwa na Japan iliyopata medali saba za dhahabu, ,bili za fedha na tatu za shaba.

Mashindano yajayo ya mwaka 2017 yatafanyika jijini London nchini Uingereza.

Mwaka huu pia, Sebastian Coe raia wa Uingereza alichaguliwa rais wa Shirikisho la raidha duniani IAAF.

Anakuwa rais wa sita wa Shirikisho hilo na kuchukua nafasi ya Lamine Diack raia wa Senegal ambaye alimaliza muda wake wa kuhudumu baada ya kuwa katika wadhifa huo tangu mwaka wa 1999.

Pamoja na hayo, Shirikisho hili la riadha liliwafungia wanaridha wa Urusi kushiriki katika mashindnao ya kimataifa kwa madai yakuwa serikali ilikuwa inaunga mkno matumizi ya dawa za kusisimua misuli.

Bondia

Ikumbukwe tu kuwa mwaka huu pia katika mchezo wa bondia kulikuwa na pambano la Kihistoria kati ya Mmarekani Floyd Mayweather na Mfilipino  Manny Pacquiao.

Pambano hili lilifanyika tarehe mbili mwezi Mei katika jimbo la Nevad nchini Marekani, ni pambano ambalo lilipewa jina pambano la Karne kitengo cha Welterweight, kuwania ubingwa wa WBA, WBC na WBO.

Mayweather aliibuka mshindi katika pambano hilo lakini Pacquiao hakuonesha kufurahsihwa na uamuzi wa majaji na kuzua mjalda kuwa huenda Mayweather alipendelewa na Majaji.

FIFA

Huu umekuwa ni mwaka mgumu kwa viongozi wa soka duniani kutokana na tuhma za ufisadi zilizowakuimba baadhi ya viongozi hao.

Mwala huu ulianza kwa klufanyika kwa uchaguzi wa urais wa FIFA, kinyanganyiro kikiwa kati ya Sepp Blatter na Mwanamflame kutoka Jordan Hussein Bin Ali.

Uchaguzi huo wa tarehe 29 mwezi Mei ulimpa ushindi Sepp Blatter aliyepata kura 133 dhidi ya Bin Ali aliyepata kura 73.

Na kabla ya uchaguzi huo viongozi wa mashtaka kutoka Marekani wakishirikiana na wale wa Zurich, walitangaza kuwafungulia mashtaka viongozi wakuu wa FIFA kwa tuhma za ufisadi.

Maafisa saba wa FIFA walikamatwa kwa tuhma za ufisadi, kabla ya kuhudhuria mkutano wa 65 wa FIFA.

Kulikuwa na madai kuwa, mbali na ufujaji wa fedha, kulikuwa na upendeleo wa mataifa ya Urusi na Qatar kuandaa kombe la dunia mwaka 2018 na 2022 lakini pia tuhma za kuhongwa kwa maafisa wa maafisa wa Kamati kuu ya FIFA kwa kombe la dunia lililofanyika nchini Ujerumani mwaka 2006 na Afrika Kusini mwaka 2010.

Lakini Terehe 2 mwezi Juni, Blatter aliitisha mkutano wa dharura katika Makao makuu ya FIFA jijini Zurich, na kutangaza kuwa atajiuzulu urais na kuitisha mkutano mwingine wa viongozi wa soka duniani kumchagua rais mpya wa FIFA.

Mwezi Oktoba wafadhili wakuu wa FIFA kama Coca Cola , ,McDonald'sna Visa  waliendelea kutoa shinikizo kwa Sepp blatter kujiuzuli kabisa katika wadhifa huo kwa tuhma hizo.

Na mwezi huo wa Oktoba Kamati ya maadili iliwapiga marufuku ya siku tisini kutojihusisha na maswala ya soka Sepp Blater na rais wa Shirikisho la soka barani Ulaya UEFA, Mitchel Platini kwa madai ya Blatter kuamuru Platini kulipwa Dola Milioni 2 malipo ambayo hayakuwa rasmi.

Hatua hiyo ilisababisha Makamu rais wa FIFA na rais wa Shirikisho la soka barani Afrika CAF Issa Hayaotue alianza rasmi kazi ya kukaimu urais wa FIFA kabla ya uchaguzi mwingine ulioratibiwa kufanyika tarehe 26 mwezi Februari mwaka 2016.

Lakini ikumbukwe kwamba Majaji wa kamati hiyo waliwapiga marufuku Blatter na Platini miaka minane ya kutoshiriki katika maswala ya soka.

Wawili hao wamesema watakata rufaa katika Mahakama ya Kimataifa ya Michezo na wanaamini kuwa hawana makosa.

Barani Afrika katika mchezo wa soka-Tanzania

Shirikisho la soka nchini Tanzania pia mwaka huu lilimfuta kazi kocha wa timu ya taifa ya soka Taifa Stars Mholanzi Mart Nooij kwa matokeo mabaya na nafasi yake kuchukuliwa na Charles Boniface Mkwasa.

Uganda....

Timu ya taifa ya soka ya Uganda, ilishinda taji la mwaka huu la CECAFA baina ya mataifa ya Afrika Mashariki na Kati iliyoandaliwa nchini Ethiopia .

Hili lilikuwa taji lao la 14 tangu kuanza kwa mashindano haya.

DRC

Klabu ya TP Mazembe ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo ilinyakua taji la klabu bingwa mwaka huu wa 2015 na kuliwakilisha bara la Afrika katika mashindano ya kombe la dunia baina ya vklabu ambao yamemaliziam mweiz huu wa Desemba nchini Japan na Barcelona kunyakua ubingwa.

Mazembe wao walifika katika hatua ya robo fainali.

Mchezo wa pete...

Katika mchezo wa pete au Netall, kwa upande wa wanawake, Uganda, Zambia, Malawi na Afrika Kusini zilifuzu katka mashindano ya kombe la dunia yaliyofanyika nchini Australia na hao ndo waliokuwa mabingwa.

Mwayi Kumwenda mchezaji kutoka Malawi aliibuka mchezaji bira katika mashindano hayo.

Uganda ilimaliza ya nane kati ya mataufa 16 yaliyishiriki katika masjhindano hayo lakini timu hiyo iligugikwa na huzuni baada ya mchezaji wake wa kutegemewa Harriet Apako kufariki dunia.

Katika mchezo wa Rugby au Raga

Kombe la dunia la mchezo wa Rugby au raga mwaka huu wa 2015, lilifanyika nchini Uingereza kati ya mwezi Septemba na October.

Mataifa 20 yalishiriki na mabingwa watetezi wakaibuka New Zeland baada ya kuwashinda Australia.

Afrika Kusini walimaliza nafasi ya tatu katka mashindano hayo.

Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.