Sport

Man United Yaichapa Schalke 04 mabao 2-0

Vijana wa Manchester United.
Vijana wa Manchester United. Reuters

Manchester United imejiweka kwenye nafasi nzuri kuelekea katika fainali ya Klabu Bingwa barani Ulaya, baada ya kuifunga Schalke04 katika nusu fainali ya kwanza nchini Ujerumani ma bao 2 kwa sufuri.

Matangazo ya kibiashara

Kipa wa Schalke 04 alitumia nguvu zake za ziada ili kuzuia mikwaju ilioelekezwa nyavuni na washambulizi wa Man U kabla ya kipindi cha kwanza kumalizika.
Manchester United walipata bao la kwanza baada ya kipindi cha pili kuanza kupitia mchezaji wake Wayne Rooney alipopenyeza mpira kwa mshambuliaji mwenzie R. Gigs na baadae kusindiria msumari kwa kupachika bao la pili.
United itaikaribisha Schalke kwenye uwanja wa Old Trafford, Jumatano tarehe 4 mwezi Mei, kwa ajili ya mchezo wa pili wa nusu fainali.
Manchester United ikidhibiti ushindi wao, basi watawakilisha soka ya England katika Fainali ya Klabu Bingwa Ulaya itakayochezwa kwenye uwanja wa Wembley.