Ligi kuu ya Uingereza

Giggs: Tutawafunga Chelsea jumapili.

Mshambuliaji wa klabu ya Manchester united ya nchini uingereza mkongwe, Rayn Giggs amesema kuwa anaimani kubwa kuwa siku ya jumapili watawafunga mahasimu wao klabu ya Chelsea katika mchezo wa ligi kuu ya nchini humo utakaopigwa katika uwanja wa Old Trafford, mchezo ambao utatoa picha halisi ya nani ataibuka bingwa msimu huu.

Mshambuliaji wa Man U, Rayn Giggs akifunga moja ya goli wakati timu yake ilipocheza na Schakle 04 ya ujerumani.
Mshambuliaji wa Man U, Rayn Giggs akifunga moja ya goli wakati timu yake ilipocheza na Schakle 04 ya ujerumani. REUTERS/Alex Domanski
Matangazo ya kibiashara

Akizungumza wakati wa mazoezi ya timu yake, Giggs amesema kuwa timu yake ina nafasi kubwa ya kuibuka na ushindi katika mchezo huo wa jumapili akijinasibu kuwa wachezaji wa timu hiyo wako katika hali nzuri kukabiliana na timu hiyo.

Picha - Chelsea na Man U

Kauli hiyo inakuja wakati zikiwa zimebaki saa chache kabla ya kushuhudia timu hizo zikishuka uwanjani kupepetana katika mchezo wa ligi kuu ambao utatoa picha halisi ya nani ataibuka na kikombe msimu huu wakati ambapo timu hizo zimetofautiana kwa pointi tatu.

Mchezo huo unabashiriwa kuwa mgumu kwa timu zote mbili, kwani ili man u waweze kutwaa ubingwa msimu huu na kujihakikishia nafasi hiyo basi ni lazima wawafunge Chelsea ili kujiweka katika nafasi nzuri zaidi ya kutangaza ubingwa mapema zaidi, endapo Chelsea watwafunga man u basi watalingana kwa pointi na kila timu itakuwa imebakiza mechi mbili ambazo zitakuwa ngumu pia kwa timu zote mbili lakini Chelsea wakipewa nafasi zaidi ya kushinda mechi zilizosalia.

Tayari makocha wa pande zote mbili wamezungumzia mchezo huo huku kila mmoja akikiri kuwa mchezo huo utakuwa mgumu kwao lakini kila timu imejiandaa vya kutosha kuhakikisha inaibuka na ushindi na hatimaye kutwaa kikombe msimu.

Wakati Chelsea wakitaka kushinda ili kutetea ubingwa wao, Manchester united watakuwa wakipambana kutaka kuweka historia ya kutwaa kikombe hicho mara nyingi zaidi nchini Uingereza kuipiku klabu ya Liverpool.