LIGI KUU ULAYA

Pazia la Ligi kuu ya Uingereza kuhitimishwa hii leo

Pazia la ligi kuu mbalimbali za mpira wa miguu barani ulaya litakuwa linafungwa leo kwa timu zinazoshiriki ligi kuu kucheza mechi zao za kukamilisha ratiba huku baadhi ya nchi tayari mabingwa wamekwishapatikana.

Matangazo ya kibiashara

Nchini Uingereza hii leo mabingwa wapya Manchester United watakuwa wanakamilisha ratiba kwa kucheza na klabu ya Blackpool katika mchezo ambo pia unatarajiwa kuwa wa kusisimua kufuatia timu zote mbili kutamba kuibuka na ushindi.

Manchester United walitawazwa mabingwa wapya juma lililopita na kufanikiwa kuweka rekodi mpya ua kulitwaa kombe la ligi kuu ya nchini Uingereza kwa mara kumi na tisa.

Mchezo mwingine unaoangaliwa sana ni ule utakao wakutanisha timu ya Manchester City ambao watakuwa ugenini kucheza na Bolton, wakati ndugu zao Arsenal watakuwa wageni wa Fulham.

Manchester City na Arsenal wote wanawania nafasi ya mshindi wa nne ambayo itatoa nafasi ya mshindi kushiriki hatua ya makundi kukata tiketi ya kushiriki fainali za kombe la klabu bingwa barani ulaya hatua ya makundi msimu ujao.

Nchini Italia pia pazia la ligi hiyo litakuwa linahitimishwa huku mabingwa AC Milani wakitangazwa juma lililopita kuwa mabingwa wapya wa ligi hiyo.

Nchini Hispania tayari FC Barcelona wameshatawazwa kuwa mabingwa wapya, wakati nchini Ujerumani timu ya Borussia Dortimundi wakiwa wamekwishatawazwa kuwa mabingwa.