Tenesi

Nadal, Wozniacki wawa vinara katika Tenesi

Rafael Nadal akisherehekea ushindi
Rafael Nadal akisherehekea ushindi Ảnh:REUTERS/Eric Gaillard

Shirikisho la mchezo wa tenesi duniani, WTA limetangaza orodha ya wachezaji wanaoongoza kwa ubora duniani katika mchezo huo.

Matangazo ya kibiashara

Kwa upande wa wanaume katika orodha hiyo mchezaji wa tenesi Rafael Nadal wa Hispania amekuwa kinara wa ubora na kuwabwaga wachezaji wengine wakati mchezi Novak Djokovic wa Serbia ameshika nafasi ya pili akifuatiwa na Rogger Federer aliyeshika nafasi ya tatu.

Mchezaji Andy Murray ameshika nafasi ya nne wakati Robin Soldering ameshika nafasi ya tano katika kinyang'anyiro hicho.

Wanawake, wao wanaongozwa kwa ubora na mchezaji Caroline Wozniacki wa Denmark akifuatiwa na Kim Clijsters wa Ubelgiji wakati Vera Zvonareva ameshika nafasi ya tatu.

Nafasi ya nne kwa upande wa wanawake imechukuliwa na Victoria Azarenka na kufuatiwa na Francesca Schiavone.