UEFA

Nani kuibuka mshindi leo kati ya Man U na Barca?

Wayne Rooney
Wayne Rooney

Kitendawili cha nani atatawazwa kuwa bingwa mpya wa kombe la klabu bingwa barani ulaya kwa mwaka 2011/2012 atajulikana muda mchache ujao.

Matangazo ya kibiashara

Tayari hivi sasa homa ya mpambano huo kwa mashabiki wa timu za manchester united na FC Barcelona tayari imepanda huku kila mmoja akimtambia mwenzake kuibuka na ushindi katika mchezo wa hii leo ambao utapigwa majira ya saa 9.45 kwa saa za afrika mashariki.

Ulinzi umeimarishwa mjini Londo ambako mchezo huo wa fainali utapigwa, huku shirikisho la mchezo huo barani ulaya UEFA likitangaza kuwa mchezo huo utavunja rekodi kwa kuwangaliwa na mashabiki wengi wa soka duniani.

Hiyo jana baadhi ya wachezaji wa pande zote mbili walipohojiwa na vyombo vya habari kila mmoja alisifu uwezo wa timu mwenza wakisema kuwa wanatarajia kuona mchezo mzuri kwakuwa wote ni mabingwa ligi za nyumbani kwao.

Macho na masikio ni kwa mchezaji bora wa dunia Lionel Messi ambaye ameonekana kuwa kinara wa ufungaji katika safu ya ushambuliaji ya Barca huku kwa upande wa manchester united kinda Javier Hernandez anapewa nafasi kubwa ya kufanya vema katika mchezo wa leo.

Wakati maandalizi ya mchezo huo yakiwa yamekamilika, tayari kuna vioja vimeibuka kuwa huenda manchester united akatwaa kikombe hicho msimu huu kufuatia utabiri wa pweza Iker wa kile nchini Hispania ktabiri hivyo.

Lakini yote tisa kumi ni mara baada ya dakika tisini ndipo mashabiki wa soka watafahamu ni nani bingwa kati ya Manchester united na Fc Barcelona.