UEFA

FC Barcelona watawazwa kuwa mabingwa wapya wa UEFA 2011/2012

Wachezaji wa Barcelona wakishangilia kutawazwa mabingwa UEFA 2011/ 2012
Wachezaji wa Barcelona wakishangilia kutawazwa mabingwa UEFA 2011/ 2012 Reuters

Hatimaye klabu ya Fc Barcelona yenye maskani yake nchini Hispania katika jiji la Barcelona, jana usiku walitawazwa kuwa mabingwa wapya wa kombe la klabu bingwa barani ulaya kufuatia ushindi wa mabao 3-1 dhidi ya Manchester United ya uingereza.

Matangazo ya kibiashara

Katika mchezo huo ambao kwa mara ya kwanza umeshuhudiwa na mashabiki wengi wa soka duniani kutokana na ukubwa wa uwanja wa Webley wa nchini uingereza na kufurika kwa mashabiki wa timu hizo kuzishabikia.

Katika mchezo huo ambao kwa takribani dakika zote tisini ulitawaliwa na Fc Barcelona, ndio waliokuwa wa kwanza kuzifumania nyavu za wapinzani wao katika dakika ya 27 ya mchezo kupitia kwa Pedro kabla ya manchester united hawajasawazisha bao hilo kupitia kwa mshambuliaji wake Wyne Rooney katika dakika ya 34 na timu hizo kwenda mapunziko zikiwa sare ya bao 1-1.

Kipindi cha pili kilianza kwa kasi ambapo walikuwa ni Barca tena kwa mara nyingine kupitia kwa mchezaji bora wa dunia kwa misimu miwili mfululizo Lionel Messi ambaye aliiandikia bao la pili timu yake katika dakika ya 54 kabla ya mchezaji David Villa hajahitimisha karamu ya mabo kwa kuandika bao la tatu na la ushindi katika dakika ya 69 na kupeleka kilio kwa mashabiki wa manchester united.

Katika mchezo huo sifa ya pekee zimwendee mshambuliaji muargentina Lionel Messi ambaye aliongoza mashambulizi ya timu yake na kuisaidia kutwaa ubingwa wa mwaka huu kwa staili ya aina yake.

Kwa muda wote wa mchezo kocha wa manchester unted mzee Alex fergason alionekana kutokuwa na furaha wala kufurahia kiwango cha wachezaji wake na kuonekana mara moja tu akisimama kutoa maelekezo kwa wachezaji wake.

Timu ya manchester united ilikuwa na:1. Edwin van der Sar 15 Nemanja Vidic 5 Rio Ferdinand 3 Patrice Evra 20 Fabio 11 Ryan Giggs 16 Michael Carrick 13 Park Ji-Sung 25 Antonio Valencia10 Wayne Rooney 14 Javier Hernández. baadae waliingia Paul Scholes kuchukua nafasi ya Michael Carrick, Luis Nani kuchukua nafasi ya Fabio.

Fc Barcelona walukuwa na: 1 Victor Valdés 3 Gerard Piqué 14 Javier Mascherano 22 Eric Abidal 2 Dani Alves 16 Sergio Busquets 8 Andrés Iniesta 6 Xavi 7 David Villa 10 Lionel Messi 17 Pedro. Baadae waliingia Seydou Keita kuchukua nafasi ya David Villa, Carles Puyol kuchukua nafasi ya Dani Alves, Ibrahim Afellay kuchukua nafasi ya Pedro.

Katika mchezo huo mchezaji Bora wa mchezo alikuwa ni Xvavi Hernandez wa Fc Barcelona.

Kwa matokeo hayo Fc Barcelona wameendelea kuudhihirishia ulimwengu kuwa wao ni timu bora kwasasa duniani, wakifanya kama walivyofanya mwaka 2009 walipowafunga manchester united kwa mabo 2-0.