Michezo, Manchester United

Paul Scholes astaafu -Manchester United.

Mchezaji wa Man U Paul Scholes
Mchezaji wa Man U Paul Scholes Allstar

Paul Scholes mchezaji wa klabu ya Manchester United, ametangaza kustaafu kwake, baada ya kujiunga na klabu hiyo tangu mwaka  1994.

Matangazo ya kibiashara

Scholes ambaye amekuwa kiungo cha kati amestafu akiwa na umri wa miaka 36 na ameichezea klabu hiyo mara 676, na sasa atajiunga na kamati ya ufundi ya klabu hiyo kama mmoja wa wakufunzi.

Tangu kujiunga na Manchester United Scholes ameisadia klabu hiyo ya London kushinda mataji kumi, licha ya kupoteza katika fainali ya klabu bingwa barani ulaya dhidi ya Barcelona mwishoni mwa juma kwa kufungwa mabao 3 kwa 1.

Scholes amesema kuwa ametafakari kwa kina uamuzi huo wa kuacha kucheza soka la kulipwa. Kocha wa Man United Sir Alex Ferguson amemsifu Scholes kwa kujitoa na kusimama na klabu hiyo kwa kipindi hicho chote.

Scholes atakumbukwa pia kustaafu kuichezea timu ya taifa ya Uingereza mwaka wa 2004, na pia atakumbukwa kwa mchango wake mkubwa katika timu hiyo ya Uingereza wakati wa kombe la dunia mwaka 1998 na 2002.