Michezo, Tennis

Mashindano ya Tennis French Open yashika kasi kuelekea robo fainali

Raphael Nadal
Raphael Nadal Rolandgaross

Mashindano ya mwaka huu ya Tennis ya French Open, yameingia katika awamu ya lala salama huku fainali ikitarajiwa kuchezwa mwishoni mwa juma hili.

Matangazo ya kibiashara

Kwa upande wa wanaume, Andy Murray wa nne kwenye oroodha duniani kutoka Uingereza anamenyana na Mserbia Victor Troicki katika raundi ya nne ya kinyanganyiro hicho ambacho kiliahirihswa jana kutokana na giza.

Hadi kuahirishwa kwa mchuano huo, Murray alikuwa anaongoza kwa seti  4-6 4-6 6-3 6-2. Andy Murray amekuwa akiuguza jeraha ,baada ya mchuano wake dhidi ya Michael Berrer kutoka Ujerumani katika raudi ya tatu ya michuano hiyo.
Katika robo fainali ya kwanza, Gael Monfils mfaransa huyu, atamkaribisha Roger Federer kutoka Uswizi wa tatu kwenye orodha ya duniani.

Kwa upande wa akina dada, Maria Sharapova kutoka Urusi wa nane kwenye orodha  atamenyana na Andrea Petkovic kutoka Ujermani katika robo fainali ya kwanza alhamisi hii, huku robo fainali nyingine ikiwa kati ya Li Na kutoka China na Victoria Azarenka kutoka Belarus.