Misri-All Africa Games

Droo ya mashindano ya All Africa Games kufanyika mjini Cairo

Droo ya timu za soka zitakazoshiriki katika makala ya kumi ya mashindano ya All Africa Games yatakayoandaliwa jijini Maputo Msumbiji, inafanyika leo Jumanne huko Cairo Misri katika makao makuu ya shirikisho la soka barani Africa CAF.

Africa-badminton
Matangazo ya kibiashara

Rais wa CAF Issa Hayatou anatarajiwa kuhudhuria hafla hiyo ,ambayo timu nane ambazo zimefuzu katika mashindano hayo, zitagawanywa kwa makundi mawili kila kundi likiwa na timu nne.

Timu mbili zitakazokuwa zimefanya vyema, zitakutana katika fainali kabla ya fainali ya kombe hilo.

Tayari wenyeji Msumbiji, Misri, Madagascar, Cameroon, Afrika Kusini na Ghana ni baadhioya timu zilizofuzu katika mashindano hayo.

Cameron ndio mabingwa watetezi.