Uingereza

Makala ya 140 ya Golf ya St.Georges yaanza.

Uwanja wa mchezo wa golf
Uwanja wa mchezo wa golf Thomas Bourdeau/RFI

Makala ya 140 ya mashindano ya Golf ya British Open yanaaza yamenza jijini London Uingereza ,huku wachezaji wengi wakihofiwa kuathiriwa na kibaridi kikali wakati wa mashindano hayo.

Matangazo ya kibiashara

Peter Dawson, mkurugenzi mkuu wa mashindano hayo amesema maandalizi yote yamekamilika na kinachosalia ni wachezaji kufika uwanjani.

Baadhi ya wachezaji wanaotarajiwa kuleta ushindani mkubwa katika mashindano hayo ni pamoja na bingwa wa mashindano ya US Open, Rory Mcllroy, kutoka Ireland na bingwa mtetezi wa mashindano haya Lousia Oosthuizen kutoka Afrika Kusini, miongoni mwa wengine.

Lam Chih Bing kutoka Singapore, anaamini kuwa huu ni mwaka wake wa kunyakua taji hili na anasema uugwanji mkono kutoka kwa familia yake unampa matumaini makubwa ya kufanya vyema.

K.J. Choi kutoka Korea naye amedokeza kuwa anatarajia kufanya vyema katika makala haya yanayokamilika siku ya Jumapili.