Zambia

Simukunda ateuliwa kuwakocha bora nchini Zambia.

CAF

Kocha wa klabu ya soka ya Zesco ya Zambia Fighton Simukonda ndiye kocha bora wa mwaka nchini humo.

Matangazo ya kibiashara

Simukonda, amepata taji hilo baada ya kuandikisha matokeo bora msimu huu na kufanikisha klabu ya Zesco United kuwa mabingwa wa ligi ya soka nchini humo mwaka 2010-2011.

Pamoja na hilo,kocha huyo ameshinda mataji matatu katika miaka sita ambayo amekuwa katika klabu hiyo na mara ya kwanza alishinda taji hilo akiwa na klabu ya Zanaco mwaka 2005.

Simukonda amewahi kufunza ,Konkola Blades FC,Roan United na Nkana FC,huku akiwa kocha msaidizi wa timu ya taifa ya Chipolopolo kati ya mwaka wa 2001 na 2008.
Jacob Banda anayeschezea ZESCO United naye alituzwa mchezaji bora wa mwaka.