MADRID-HISPANIA

Real Madrid FC na FC Barcelona kumaliza ubishi Jumatano hii

Danny Alves wa Barcelona akichuana na Christian Ronaldo wa R. Madrid
Danny Alves wa Barcelona akichuana na Christian Ronaldo wa R. Madrid Online

Klabu ya FC Barcelona na Real Madrid zote za nchini Hispania zinatarajiwa kukutana tena kwa mara ya pili siku ya Jumatano katika mechi ya kuwania Super Cup, mtanange utakaopigwa katika dimba la Camp Nou.

Matangazo ya kibiashara

Siku ya Jumapili timu hizo zilikutana katika dimba la Santiago bernabeu na kushuhudia zikitoshana nguvu kwa kufungana mabao 2-2 katika mchezo uliokuwa mkali na wakusisimua kwa muda wote wa mchezo huku shukrani zikimwendea Xabi Alonso kiungo wa R. Madridi kwakuisawazishia bao timu yake.

Real Madrid ndio waliokuwa wa kwanza kupata bao kupitia kwa Mesut Ozil kabla ya David Villa kuisawazishia timu yake na kufanya matokeo kuwa bao 1-1.

Mchezaji bora wa dunia Lionel Messi ndiye aliyeifungia timu yake bao la pili baada ya kuwazidi ujanja mabeki wa Madrid lakini hata hivyo bao lake halikudumu sana kwani Xabi Alonso aliisawzishia timu yake bao na kufanya mchezo huo kwenda kumaliza ubishi katika dimba la Camp Nou, Barcelona.

Nchini Uingereza ligi hiyo imeendelea siku ya Jumapili kwa michezo kadhaa kupigwa ambapo mabingwa watetezi klabu ya Manchester United walikuwa wageni wa West Brownich Albion na kufanikiwa kuibuka na ushindi wa mabao 2-1 huku sifa zikimwendea kiungo mshambuliaji Ashley Young aliysajiliwa msimu huu na klabu hiyo.

Matajiri wa jiji la London kalbu ya Chelsea ikiwa chini ya kocha wake mpya Villas Boaz ilijikuta ikilazimishwa sare ya bila kufungana na klabu ya stoke City.

Ligi hiyo inatarajiwa kuendelea tena jumatatu hii kwa vinara manchester City kucheza na timu ngeni ya Swansea.