Ligi kuu ya Uhispania

José Mourinho. akanusha habari za kuipa kisogo klabu yake ya Real Madrid

Meneja wa klabu ya Real Madrid José Mourinho.
Meneja wa klabu ya Real Madrid José Mourinho. Reuters

Kocha Mkuu wa Real Madrid ambaye amebarikiwa kuwa na mbwembwe nyingi na maneno chunumzima José Mourinho ameandika barua ta wazi kwa mashabiki wake na kutupilia mbali uvumi uliokuwa umezagaa ya kwamba anataka kuipa kisogo klabu hiyo.

Matangazo ya kibiashara

Hatua ya Mourinho kuandika barua imekuja baada ya kuwepo kwa taarifa kutoka kwenye vyombo vya habari zikieleza kuwa Kocha huyo hana raha kutokana na kutopata msaada anaouhitaji kutoka Bodi ya klabu hiyo.

Mourinho ambaye kwa sasa anachunguzwa na Chama Cha Soka nchini Uhispania kwa vitendo alivyovifanya kwenye mchezo wa Super Cup dhidi ya Barcelona amesema watu wamekuwa wakizungumza mengi lakini yeye mwenyewe ndiyo anajua ukweli.