Ligi ya mabinwa Barani Ulaya

Kocha wa Man City asema yeye na Tevez sasa basi

Kabla ya dakika 35 mchezo kumalizika Manchester City ilikuwa imelazwa kwa mabao 2 kwa bila. Kocha wa Man City alimtaka Tevez kuingia uwanjani ili asaidie kuokoa jahazi la Man City. Tevez akakataa kutii amri ya kocha wake.Mancini alisema kuwa "yeye na Tevez wamemalizana”.

Matangazo ya kibiashara

Carlos Tevez kwa muda sasa Teves amekuwa akitishia kuihama klabu hiyo kwa madai ya kutaka kuwa karibu na familia yake lakini hadi sasa hajafaulu.

Na msimu huu wa ligi ya uingereza ilipoanza Meneja Mancini alimpokonya Teves unahodha na kumkabidhi Viny Kompany wadhifa huo.

Katika mechi nyengine ya kombe hilo Manchester United iliponea chupuchupu wakati wakikutana na Basel kwenye uwanja wa Old Trafford.

Man U waliokuwa wanaongoza kwa magoli mawili kwa sufuri katika kipindi cha kwanza waliona Basel wakikomboa magoli yote katika kipindi cha pili na halafu kuongeza goli la tatu.

Iliilazimu Man U kupigana kufa na kupona hadi dakika ya mwisho ilikukomboa goli hilo la tatu kupitia mchezaji Ashley Young.

Kwengineko Real Madrid ilichuna Ajax Amsderdam ya uholanzi magoli 3-0.
Magoli hayo yalifungwa katika kipindi cha kwanza na Cristiano Ronaldo, Kaka and Karim Benzema .

Inter Milan ikiwa ugenini iliifunga CSK Moscow 3-2 Kwa upande mwingine Villareal ya uhispania waliabishwa katika uwanja wao wa nyumbani walipo dungwa 2-0 na Napili ya Italy.

Leo usiku itakuwa zamu ya Arsenal kuikaribisha Olympiakos huko Emirati huku mabingwa watetezi wa kombe hilo FC Barcelona wakisafiri kumenyana na Barisov na Velencia ikiwaalika Chelsea.