UFARANSA

Nasri asaidia Ufaransa kufuzu fainali ya soka barani Ulaya 2012

Samir Nasri (Kushoto wa Ufaransa) akimenyana na mchezaji wa Bosnia
Samir Nasri (Kushoto wa Ufaransa) akimenyana na mchezaji wa Bosnia REUTERS/Benoit Tessier

Samir Nasri, aliipa ufaransa bao muhimu kupitia mkwaju wa penalti dhidi ya Bosnia, katika mchuano wa mwisho wa kuwania nafasi ya kushiriki katika fainali ya mashindano ya soka baina ya matufa ya bara ulaya yatakayofanyika mwaka ujao nchini Ukraine na Poland.

Matangazo ya kibiashara

Mshambulizi wa Bosnia Edin Dzeko ndiye aliyekuwa wa kwanza kuipa Bosnia bao la kwanza katika dakika ya arobaini katika kipindi cha kwanza kabla ya kwenda katika kipindi cha mapumziko, huku Ufaransa ikijipatia bao lake kupitia kwa Samir Nasri kupitia mkwaju wa penalti,baada ya kuchezewa vibaya na Emir Spahic karibu la lango la Bosnia.
 

Ufaransa ilimaliza ya kwanza katika kundi la D kwa alama 21,ikifuatwa na Bosnia kwa alama 20, huku kocha wa Ufaransa Laurent Blanc akisema kuwa wachezaji wake walicheza chini ya kiwango alichotarajia hasa katika kipindi cha kwanza.
 

Wenyeji Poland na Ukraine wanafuzu moja kwa moja,huku timu tisa zinazoongoza makundi yao zikifuzu pia, huku timu ya pili katika kila kundi iliyo na alama nyingi ikifuzu pia,timu ambazo tayari zimefuzu ni pamoja na ufaransa, Ujerumani, Urusi, Italia, Uingereza,Holland, Denmark na Uhispania.
 

Kinyanganyiro cha mwaka ujao, ndicho kitakachokuwa cha mwisho kuyakutanisha mataifa 16 ya bara uala baada ya viongozi wa UEFA kuafikiana kuongeza mataifa yatakayoshiriki katika fainali zijazo kufikia 24, kuanzia fainali ya mwaka 2016 itakayoandaliwa nchini Ufaransa.