AFCON

Uchambuzi wa mataifa kongwe yaliyobanduliwa nje ya fainali ya kombe la mataifa bingwa barani Afrika 2012

CAF

Uchambuzi wa Mataifa kongwe yaliyobanduliwa nje ya mashindano ya kuwania ubingwa wa mataifa bora barani Afrika katika mchezo wa soka,fainali zitakazofanyika mwaka 2012 nchini,Gabon na Equitorial Guinea.

Matangazo ya kibiashara

Kinyanganyiro cha kusaka tiketi ya kufuzu katika fainali ya soka ya mataifa bingwa barani Afrika mwaka 2012 nchini Gabon na Equitorial Guinea kilimazika ,huku mataifa kongwe zilibabduliwa nje ya fanali hiyo.

Afrika Kusini.

Bafana Bafana ya Afrika Kusini,iliyoshindwa kufuzu mbele ya Niger katika kundi moja kila timu ikimaliza kwa alama 9,ikiwemo Siere Leone lakini kulingana na mechi kati ya timu hizo mbili Niger ilionekana kufanya vyema,huku sheria za CAF,zikitumika kupata mshindi amabye alikuwa ni Niger.

Sheria za CAF zinaeleza kuwa hali kama hiyo inapotokea kwa timu mbili au tatu katika kundi moja,kwa kutishanana kwa alama,timu itakayofuzu ni ile itakayokuwa imefunga mabao mengi baina ya timu zinazowania nafasi hiyo ya kufuzu.

Afrika Kusini,ilijaribu kukataa rufaa katika shirikisho la soka barani Afrika kutaka uamuzi wa CAF kubadilishwa kwa madai kuwa walikuwa na mabao mengi kuliko Niger,lakini hawakufaulu kutokana na sheria za CAF.

Wachambuzi wa soka wanaona kuwa,sare ya Bafana Bafana ya kutofungana na Siere Leone ndio iliyowasabisha wao kutofuzu katika fainali hizo.

ALGERIA
 

Algeria ilishiriki katika katika fainali ya kombe la dunia mwaka 2010 nchini Afrika Kusini,na katika kundi lao ilimaliza ya nne.
 

Walipoanza kampeni zao walitoka sare ya bao moja kwa moja na Tanzania matokeo ambayo yalisukuma shirikisho la soka nchini humo,kumfukuza kocha wao Rabah Saadane.
 

Mkufunzi mpya Abdelhak Ben Chikha alichukua ukufunzi wa Algeria na katika mchuano wao wa ugenini mjini Bagui,walichabangwa na Jamhuiri ya Kati kwa mabao 2 bila jibu,kabla ya kugaragazwa na Morrocco kwa mabao 4 kwa bila.
Na hivyo,Algeria ilimaliza katika nafasi ya tatu kwa alama nane.

NIGERIA
 

Nigeria pia ilishiriki katika kombe la dunia mwaka 2010 nchini Afrika Kusini,na kuajiriwa kwa kocha mpya, kuliwapa matumaini makubwa wapenzi wa soka nchini humo kwa kuwepo kwa kocha wa nyumbani hatimaye angewafikisha vijana wa Super Eagles huko Gabon na Equitorial Guinea.
 

Katika mchuano wao wa kwanza ugegeni,wealipoteza kwa bao moja kwa bila dhidi ya Guinea,kabla ya kupata sare ya mabao mawili kwa mawili dhidi ya Ethiopia jijini Addis Ababa.
 

Kutokana na matokeo hayo,vijana wa Super Eagles walimalizika katika nafasi ya tatu kwa alama 11 licha kufanya vyema dhidi ya Madagascar.

Swali ambalo wengi wanajiuliza ni ikiwa,shirikisho la soka nchini Nigeria litampiga kalamu kocha wao Samson Siasia kwa kushindwa kuwafikisha vijana hao huko Guinea Bissau na Gabon mwaka 2012.

CAMEROON
 

Wachambuzi wa soka wanaona kuwa ikiwa vijana wa Indomitable Lions wangekuwa katika kundi lingine wangefuzu katika kinyanganyiro hicho,lakini kutokana na kujumuihswa na wapinzani wao wa jadi Senegal katika kundi moja,huenda mambo hayakuwa mazuri kwao.
 

Walianza kwa kupoteza jijini Dakar Senegal kwa kufungwa bao moja kwa bila kabla ya kutoka sare ya bila kwa bila nyumbani kwao jijini Yaounde, na pia kutoka sare nyingine ya bila kwa bila na Jamhuri ya Kidemokrasaia ya Kongo,matokeo amabyo yalisabisha vijana hao wa Indomitable Lions kumaliza nyuma ya Senegal kwa alama 11 na hivyo kushindwa kufuzu kwa fanaili hizo.

MISRI
 

Misri ndio mabingwa watetezi wa kombe hili la matifa bingwa barani Afrika, na wameshinda mara tatu mfululizo,na wakati wa kampeni hizo ilidhaniwa kuwa wagechukua uongozi wa kundi lao kwa urahisi mno.
 

Pharaohs kama wanavyojulikana walianza kampeni hizo kwa kutoka sare ya kufungana bao moja kwa moja na Sierra Leone jijini Cairo,na baadaye kupoteza kwa bao moja kwa bila dhidi ya Niger,matokeo yaliyowashangaza wapenzi wa soka nchini Misri na barani Afrika ,hata hivyo kufungwa na Bafana Bafana ya Afrika Kuisni bao moja kwa bila ,iliashiria kuwa mabingwa hao kufuzu katka mashindano hayo ya mwaka 2012 haingekuwa rahisi.
 

Misri ilimaliza ya mwisho katika kundi lao,lililojumuisha Afrika Kusini, Niger na Siere Leone na hivyo kumaliza kwa alama 5.
 

Kutokana na matokeo hayo mabaya, shirikisho la soka nchini Misri lilimfuta kazi kocha wao wa siku nyingi Hassan Shehata.