Fainali - Rugby

Craig Joubert kutoka afrika Kusini kucheza fainali za Rugby

Mpuliza kipenga wa Afrika ya kusini Craig Joubert ameteuliwa kuchezesha mchezo wa fainali siku ya jumapili kati ya wenyeji New Zealand na Ufaransa mchezo utakao pigwa katika dimba la Eden Park.

RugbyRama
Matangazo ya kibiashara

Uamuzi huo umetolewa na tume ya uteuzi ya mchezo wa Raga mjini Auckland hii leo baada ya kupitia kwa kina uwezo wa wapuliza vipenga katika michezo iliyopita ambapo Craig Joubert ameonesha uwezo wa kipekee katika kusimamia vizuri mchezo wa nusu fainali kati ya New Zealand na Australia mwishoni mwa juma.

Craing anaingia katika historia ya Afrika kusini kuwa m Afrika kusini wa pili kuchezesha fainali za kombe la dunia akimfuatia Andre Watson ambaye enzi zake aliwahi kuchezesha kombe la dunia mara mbili.

Joubert ataungana na refarii aliye chezesha fainali hizo mwaka 2007 Alain Rolland wa Ireland na Nigel Owens wa Wales ambao watakuwa wasaidizi wake na Giulio De Santis wa Italy atakuwa upande wa television hata hivyo Rolland atakuwa refarii wa akiba.