Afrika kusini

Waziri wa michezo wa Afrika Kusini kumtaja mchunguzi wa kashfa ya tuzo ya ziada ya mchezo za Kriket

OFM

Waziri wa michezo wa Afrika kusini Fikile Mbalula jumahili anatarajiwa kumtaja jaji mstaafu ambaye atafanya uchunguzi wa kashfa ya tuzo za ziada ambayo imekuwa ikiichafua bodi ya taifa ya mchezo wa Kriket. 

Matangazo ya kibiashara

Maofisa wa mchezo wa Criket nchini humo CSA wamemtupa kando rais wa bodi hiyo Mtutuzeli Nyoka ambaye ameitwa mara kadhaa kwa mahojiano binafsi kuhusu kutoa tuzo za ziada kwa siri, wakati nchi hiyo ilipokuwa mwenyeji wa michuano ya kimataifa ya Kriket.

Waziri huyo amesema kuwa ataendela na uchunguzi wa suala hilo ikiwa ni njia ya kupambana na rushwa pamoja na kwamba amepokea vitisho kutoka kwa mtu asiyemfahamu akimtaka kuachana na suala hilo.

Kashfa hiyo imesababisha mchezo wa kriket nchini humo kukosa wafadhili