INDIA-FORMULA ONE

Sebastian Vettel aendelea kudhihirisha kuwa yeye ni dereva bora duniani katika mbio za Formula One

Dereva kinda Sebastian Vettel anaeitumikia kampuni ya Redbull ameendelea kung'ara vilivyo baada ya siku ya jumapili kuibuka mshindi katika mbio za magari ya Formula One yaliyofanyika nchini India.

Sebastian Vettel akishangilia moja ya ushindi wake
Sebastian Vettel akishangilia moja ya ushindi wake Reuters
Matangazo ya kibiashara

Mashindano hayo ambayo yalivuta hisia za mashabiki wengi wa mchezo huo walishuhudia kinda hiyo akiendesha gari yake kwa umakini na kuwaacha madereva wenzake umbali mkubwa.

Mashindano hayo ambayo yaliandaliwa nchini India kwa mara ya kwanza yamepongezwa na wakuu wa shirikisho la mchezo ambao awali walikuwa na hofu kuwa huenda yasingependeza kutokana na sifa mbaya ambayo India inayo katika kuandaa mashindano ya kimataifa.

Katika mbio hizo zilimshuhudia pia dereva Felipe Massa akipewa adhabu Lewis Hamilton.

Msimamo wa madereva katika mbio hizo ni: 1. Sebastian Vettel (GER/Red Bull), 2. Jenson Button (GBR/McLaren), 3. Fernando Alonso (ESP/Ferrari), 4. Mark Webber (AUS/Red Bull), 5. Michael Schumacher (GER/Mercedes GP).