New Zealand

Kocha wa timu ya taifa ya Rugby nchini New Zealand atangaza kujiuzulu

Kocha wa timu ya taifa ya Rugby nchini New Zealand Graham Henry
Kocha wa timu ya taifa ya Rugby nchini New Zealand Graham Henry rct

Kocha Mkuu wa Timu ya Taifa ya Rubgy ya New Zealand ambao ni mabingwa wa dunia kwenye mchezo huo Graham Henry ametangaza kujiuzulu baada ya kuweza kuinoa timu hiyo kwa kipindi cha miaka minane.

Matangazo ya kibiashara

Henty mwenye umri wa miaka sitini na tano amesema inatosha kwake ni inafaa kwa Kocha mwingine kuchukua jukumu la kuendelea mchezo wa rugby katika nchi hiyo iliyofanikiwa kutwaa ubingwa wake wa pili wa dunia baada ya kuifunga Ufaransa.

Henry amesema anajisikia faraja kwa kile ambacho amekifanya kwa New Zealand huku akiwa na rekodi ya kushinda michezo themanini na nane kati ya mia moja na tatu na hivyo kuwa ni kocha mwenye uwezo mkubwa kuweza kuifundisha All Blacks.