LIGI KUU YA UINGEREZA

Chelsea yaendelea kufanya vibaya kwenye ligi kuu ya Uingereza

Mchezaji wa Liverpool Glen Johnson akifunga bao la pili na laushindi kwa timu yake
Mchezaji wa Liverpool Glen Johnson akifunga bao la pili na laushindi kwa timu yake Reuters

Klabu ya Chelsea ya Uingereza mwishoni mwa juma imeendeleza uteja wake kwa klabu ya Liverpool baada ya kukubali kichapo cha magolo mawili kwa moja wakiwa nyumbani katika dimba la stamford Bridge.

Matangazo ya kibiashara

Katika mchezo huo ambao ulikuwa mkali na wakusisimua kwa muda wote wa mchezo uliwashuhudia vijana wa Kenny Dalglish wakiwa wa kwanza kupata bao kupitia kwa Maxi Rodriguez baada ya mchezaji wa Chelsea Mikel Obi kushindwa kuumiliki mpira na kupokonywa.

Kipindi cha pili Chelsea walifanya mabadiliko ambayo yalizaa matunda baada ya mchezaji wake kinda Daniel Sturridge kuingia na kuisawzishia bao timu yake na kufanya matokeo kuwa sare ya bao moja kwa moja.

Mchezo ulibadilika baada ya bao hilo kurejeshwa ambapo Chelsea walianza kuliandama lango la Liverpool lakini ngome ngumu ya vijana wa Dalglish iliwafanya Chelsea washindwe kupenya kupata bao la ushindi.

Wakati dakika zikiwa zimeyoyoma beki wa kushito Glen Johnson ambaye pia aliwahi kukipiga na klabu hiyo alifanikiwa kuipatia timu yake ya liverpool bao la ushindi baada ya kuwazidi ujanja mabeki wa Chelsea na kuukwamisha mpira wavuni na kubadili matokeo kuwa 2-1.

Kocha wa Chelsea Villas Boas ameonesha kusikitishwa kwake na matokeo hayo huku akiwashushia lawama nzito wachezaji wake kwa kushindwa kupata mabao huku kwa upande wa kocha wa liverpool Kenny Dalglish akikisifu kikosi chake kwa kucheza vizuri.