Pata taarifa kuu
KOMBE LA MATAIFA BINGWA BARANI AFRIKA

Timu zajipanga kwa mashindano ya soka ya mataifa bingwa barani Afrika,waamuzi watajwa

© AFP/Sia Kambou
Ujumbe kutoka: RFI
2 Dakika

Mataifa kumi na sita yatakayoshiriki katika mashindano ya soka ya mataifa bingwa barani Afrika huko Gabon na Equatorial Guinea yako katika awamu ya lala salama ya maandalizi ya mashindano hayo yatakayoanza tarehe 21 mwezi huu.

Matangazo ya kibiashara

Mataifa yaliyofuzu katika makala  haya ya 28 ya mashindano hayo ni pamoja na wenyeji Equitorial Guinea na Gabon, Bostwana, Libya, Senegal, Zambia, Cote dvoire, Sudan, Burkina Faso, Angola, Niger, Moroco,Tunisia, Ghana, Mali na Guinea.
 

Timu ya Cote Dvoire tayari imetaja kikosi chake cha awali cha wachezaji 25, ambacho kitakuwa kinapiga kambi Abu Dhabi katika mmiliki za kiarabu.
 

Wachezaji wa Ivory Coast wanaocheza soka ya kulipwa barani Ulaya hasa nchini Uingereza wamelazimika kujiunga na wenzao kwa maandalizi ya michuano hiyo,huku Yaya Toure na Kolo Toure wanaochezea klabu ya Manchester City,wakilazimishwa kuja mapema na kukosa mchuano wa kombe la FA dhidi ya Manchster United.
 

Timu nyingine ambayo pia imetaja kikosi chake cha awali ni Morrocco,ambayo imewajumuisha wachezaji watatu wanaocheza soka ya kulipwa nyumbani.
 

Vijana wa Atlas Lions wanapiga kambi mjini Marbella nchini Uhispania, wanakotarajiwa kucheza mchuano wa kujipima nguvu dhidi ya klabu ya Grasshoppers kabla ya kuelekea Gabon kwa mashindano hayo ambayo wamejumishwa pamoja na wenyeji Gabon, Tunisia na Niger.
 

Cameroon,Misri,Nigeria na Algeria ni baadhi ya mataifa yaliyoshindwa kufuzu katika mashindano hayo huku ukanda wa CECAFA, Afrika mashariki na kati ukiwakilishwa na Sudan.

Kwingineko,shirikisho la soka barani Afrika CAF limetoa orodha ya waamuzi 18 na wasaidizi 21 wakaochezesha mechi hizo.
 

Nchi ya Algeria na Cameroon ambazo hazikufuzu katika mashindano hayo ndizo zillizotoa idadi kubwa ya waamuzi hao ikiwa ni watatu kutoka kila nchi.
 

Waamuzi hao pamoja na wasaidizi wao ni pamoja na-
 

Marefarii : Maillet Eddy Allen (Seychelles), Seechurn Rajindraparsad (Mauritius), Abdel Rahman Khalid (Sudan), Daniel Bennett (Afrika Kusini ), Benouza Mohamed (Algeria), Diatta Badara (Senegal), Coulibaly Koman (Mali), Gassama Bakary Papa (Gambia), Alioum Neant (Cameroon), El Ahrach Bouchaib (Morocco), Doue Noumandiez Desire (Cote d’Ivoire), Lemghaifry Aly (Mauritania), Jedidi Slim (Tunisia), Haimoudi Djamel (Algeria), Otogo-Castane Eric Arnaud (Gabon), Sikazwe Janny (Zambia), Nampiandraza Hamada el Moussa (Madagascar), Grisha Ghead (Misri)
 

Wasaidizi: Hassani Bechir (Tunisia), Damoo Jason Joseph (Ushelisheli), Edibe Peter Elgam (Nigeria), Menkouande Evarist (Cameroon), Champiti Moffat (Malawi), Range Aden Marwa (Kenya), Siwela Zakhele Thusi (Afrika Kusini), Kabanda Felicien (Rwanda), Birumushahu Jean-Claude (Burundi), Bouende-Malonga Richard (Congo), Ogbamariam W. Angesom (Eritrea), Doumbouya Aboubacar (Guinea), Moussa Yanoussa (Cameroon), Yeo Songuifolo (Cote d’Ivoire), Camara Djibril (Senegal), Achik Redouane (Morocco), Vinga Theophile (Gabon), Diarra Balla (Mali), Etchiali Abdelhak (Algeria), Bootun Balkrishna (Mauritius), Shaanika David (Namibia)

 

 

Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.