Pata taarifa kuu
UINGEREZA

Chama Cha Soka Nchini Uingereza FA kumfungia Balotelli michezo minne

Ujumbe kutoka: Nurdin Selemani Ramadhani
1 Dakika

Mshambuliaji wa Kimataifa wa Italia ambaye anakipiga katika Klabu ya Manchester City Mario Balotelli ameingia matatani na huenda Chama Cha Soka nchini Uingereza FA kikamsimamisha kucheza michezo minne kwa kitendo cha utovu wa nidhamu mchezoni.

Matangazo ya kibiashara

Balotelli ameingia matatani baada ya picha za video kuonesha akimkanyaga kwa maksudi Kiungo wa Kimataifa wa Uingereza anayecheza Klabu ya Tottenham Scott Parker kwenye mchezo wao uliopigwa siku ya jumapili.

Balotelli alifanya kitendo hicho kwenye mchezo wao wa jumapili na timu yake ya Manchester City kufanikiwa kuibuka na ushindi wa magoli 3-2 huku goli la ushindi lililofungwa kwa mkwaju wa penalty akilifunga yeye.

Kocha wa Tottenham Harry Redknapp alichukukizwa sana na kitendo hicho cha Balotteli cha kumkanyaga Parker na mwamuzi Howard Webb ambaye alikuwa karibu kabisa na tukio hilo hakuchukua hatua zozote.

Taarifa ambayo imetolewa na Chama Cha Soka nchini Uingereza FA imethibitisha kutaka kumchukulia hatua za kinidhamu Balotteli kwa kitendo hicho ambacho si cha kiungwana michezoni.

Chama Cha Soka FA kimesema Balotelli anayo nafasi ya kukata rufaa kupinga uamuzi huo lakini iwapo mchezaji huyo atashindwa kwenye rufaa yake ni wazi adhabu yake ikaongezwa zaidi.

Balotelli amepewa adhabu ya kuwa nje kwa michezo minne kutokana na kuwa miongoni mwa wachezaji ambao tayari wameshapewa kadi nyekundu mwaka huu na hivyo nyongeza ya mechi moja lazima itolewe.

Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.