Pata taarifa kuu
EQUATORIAL GUINEA-GABON

Gabon na Tunisia wapata ushindi kwenye michezo yao ya Kundi C

Ujumbe kutoka: Nurdin Selemani Ramadhani
1 Dakika

Timu ya Taifa ya Tunisia imefanikiwa kupata ushindi mbele ya wapinzani wao Morocco kwa kuwachabanga magoli 2-1 katika mchezo wa pili wa Kundi C kwenye Mashindano ya Kombe la Mataifa ya Afrika.

Matangazo ya kibiashara

Tunisia ndiyo walikuwa wa kwanza kupata goli kupitia kwa Saber Khalifa akiunganisha faulo iliyopigwa na Khaled Korbi katika kipindi cha kwanza cha mchezo na kuwafanya waende mapumziko wakiwa wanaongoza.

Kipindi cha pili kilikuwa kigumu kwa pande zote lakini ni Tunisia kwa mara nyingie ndiyo walifanikiwa kuandika goli la pili katika dakika ya sabini na saba kupitia kwa Youssef Msakni ambaye alitokea benchi.

Morocco haikukata tamaa na badala yake iliendeleza mashambulizi langoni mwa Tunisia na katika dakika ya themanini na sita Nahodha Houcine Kharjah akafanikiwa kuwapatia goli la kufutia machozi.

Kocha Mkuu wa Tunisia Sami Trabelsi baada ya mchezo alisema ushindi huo ulikuwa muhimu sana kwao lakini mashindano bado ni magumu na wataendelea kuhakikisha wanafuzu katika robo fainali.

Mchezo wa awali ulishuhudia wenyeji wenza Gabon wakipata ushindi mbele ya Rais Ali Bongo na mkewe ambao waliongoza mashabiki wengine elfu arobaini katika Jiji la Libreville kwa kuwafunga Niger kwa magoli 2-0.

Magoli ya wenyeji yalikwamishwa nyavuni na Pierre-Emerick Aubameyang na Stephane Nguema na hivyo kujiweka katika mazingira mazuri ya kuweza kusonga mbele kwenye hatua ya robo fainali.

Kocha wa Gabon Gernot Rohr amesema huu ni mwanzo kwa hiyo atahakikisha kikosi chake kinaendelea kupambana kwenye michezo yake miwili ambayo imesalia na kutumia vyema uwenyeji wao.

Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.