UHISPANIA

Mourinho asema wachezaji wake wanaamini haiwezekani kuifunga Barcelona ikiwa Nou Camp

Kocha Mkuu wa Klabu ya RealMadrid Jose Mourinho amesema baadhi ya wachezaji wake wanaamini kuwa ni vigumu kupata ushindi mbele ya Barcelona hasa ukicheza nao kwenye Dimba la Nou Camp.

Matangazo ya kibiashara

Kauli ya Mourinho ameitoa baada ya kushuhudia Klabu yake ya Reald Madrid ikiondolewa kwenye Kombe la Copa Del Rey baada ya kuambulia sare ya magoli 2-2 kwenye mchezo uliopigwa usiku wa jana.

Mourinho amesema aliwasikia wachezaji wake wakisema kuwa haiwezekani kuwafunga Barcelona ukiwa unacheza nao kwenye Uwanja wa Nou Camp hata kama mkicheza vizuri zaidi yao.

Real Madrid walielekea kwenye Dimba la Nou Camp wakiwa na kumbukumbu ya kufungwa mchezo wa kwanza kwa magoli 2-1 kwenye Uwanja wake wa nyumbani wa Santiago Bernabeu llakini walikuja wanaambulia sare kwenye mchezo hio wa pili.

Barcelona walikuwa wa kwanza kupata goli kupitia kwa Pedro kalba ya Dani Alaves kupachika goli la pili ambalo lilidumu hadi mapumziko huku wachezaji wa Real Madrid wakijikuta wakipata kadi za njano.

Kipindi cha pili Real Madrid ilifanikiwa kurudi kwa nguvu na kusawazisha goli la kwanza kupitia kwa Cristiano Ronaldo kabla ya Karim Benzema kufunga goli la pili matokeo ambayo yalidumu hadi mwisho wa mchezo.

Real Madrid ililazimika kumaliza ikiwa na wachezaji kumi baada ya Sergio Ramos kulimwa kadi nyekundu huku timu hiyo ikipata kadi nane za njano kwa makosa ambayo Mourinho anayashakia.

Mourinho amesema kuwa tangu akiwa Chelsea, Inter Milan na sas madridi hajawahi kuona mabadiliko ya maamuzi ukicheza na Barcelona na amesema anawapongeza kwa walichokifanya Bernabeu lakini si kwa kufuzu hatua ya fainali.

Naye Kocha wa Barcelona Pep Guardiola amesema ni kweli Madrid walicheza vizuri zaidi na hakika ulikuwa mchezo mzuri na haiwezekani ukaifunga timu hiyo katika michezo miwili mfululizo.