Pata taarifa kuu
GABON-GINE YA IKWETA

Sudan yafuzu hatua ya robo fainali kombe la AFCON kwa mara ya kwanza katika kipindi cha miaka 42

Mohamed Abdullah, kocha wa timu ya taifa ya Sudan akishangilia na wachezaji wake baada ya kufanikiwa kufuzu hatua ya robo fainali
Mohamed Abdullah, kocha wa timu ya taifa ya Sudan akishangilia na wachezaji wake baada ya kufanikiwa kufuzu hatua ya robo fainali CAF Online
Ujumbe kutoka: Emmanuel Richard Makundi
2 Dakika

Kwa mara ya kwanza timu ya taifa ya Sudan imeshinda mchezo wake wa kwanza katika mashindano ya kombe la mataifa ya Afrika katika kipindi cha zaidi ya miaka 42 na kufanikiwa kusonga mbele kwenye hatua ya robo fainali ya michuano hiyo.

Matangazo ya kibiashara

Sudan imefanikiwa kufuzu kufuatia timu iliyokuwa inapewa nafasi ya kusonga mebele kwenye hatua hiyo, timu ya taifa ya Angola kushindwa kufua dafu mbele ya timu ya taifa ya Cote d'Ivoire.

Angola ambayo ilikuwa inahitaji suluhu dhidi ya Cote d'Ivore ili iweze kusonga mbele, ilijikuta ikipoteza mchezo wake baada ya kukubali kipigo cha mabao 2-0 toka kwa tembo wa Cote d'Ivoire ambao waliutawala vema mchezo wa jana.

Sudan ambayo ilikuwa haipewi nafasi ya kusonga mbele kwenye mechi ya jana, ilikuwa inacheza na timu ya taifa ya Bukinafaso na kufanikiwa kupata ushindi wa mabao 2-1 na hivyo kulingana alama na timu ya taifa ya Angola ambayo sasa imeshindwa kufuzu kutokana na tofauti ya magoli ya kufunga na kufungwa.

Sudan imefunga magoli manne sawa na Angola lakini wakatofautiana kwenye magoli ya kufungwa kwani Angola wamefungwa mabao 5 wakati Sudana wamefungwa magoli 4.

magoli ya Sudan yalifungwa na Mudathir El-Tahir aliyefunga magoli yote mawili wakati lile la Bukinafaso likifungwa na Issiaka Ouedraogo.

Hii leo michuano hiyo itaendelea ambapo timu ya taifa ya Niger watacheza na timu ya taifa ya Morocco, wakati Gabon wao watawakaribisha Tunisia katika mchezo mwingine ambao unatarajiwa kuwa wa vuta nikuvute.

Katika kundi hili tayari Tunisia na gabon zimeshafuzu kwa hivyo mchezo wa leo utakuwa ni kutafuta nani atakuwa kinara wa kundi C.
 

Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.