UINGEREZA

Tambo za Arsenal zayeyuka baada ya kupigwa 4-0 na AC Milan

RFI

Matumaini ya Klabu ya Arsenal Uingereza katika Ligi ya Mabingwa wa Ulaya jana yalififia baada ya kukubali kipigo cha mabao 4-0 kutoka kwa klabu ya AC Milan ya Italia.

Matangazo ya kibiashara

Katika mchezo huo uliovuta hisia za mashabiki wengi wa soka, Kevin-Prince Boateng alipopachika bao la kwanza huku mshambuliaji wa zamani Manchester City Robinho akipachika bao la pili na la tatu.

Penati iliyopigwa na Zlatan Ibrahimovic ilitosha kuizamiasha Arsenal na kuambulia kipigo hicho kibaya kilichotibua matumaini ya Klabu hiyo ya Uingereza.

Mapema Kocha wa Arsenal, Arsenne Wenger alikaririwa na vyombo vya habari akijigamba kuwa timu yake ingeishikisha adabu AC Milan lakini mambo yakawa tofauti na walivyotarajia.