UINGEREZA

Chelsea yamtema Andre Villa Boaz

guardian.co.uk

Kufuatia kupoteza mchezo wake wa jana dhidi ya West Bromwich, Klabu ya Chelsea imemtimua kazi kocha wake kijana Andre Villa Boaz saa 24 baada ya mchezo huo.

Matangazo ya kibiashara

Katika taarifa ilitotolewa na klabu hiyo hii leo timu ya Chelsea ambayo inashiriki ligi kuu ya Uingereza, imeamtema kocha Ander Villa Boaz na nafasi yake kwa sasa itachukuliwa na kocha msaidizi Roberto Di Matteo hadi mwisho wa msimu .

Andre Boaz mwenye umri wa miaka 34 amejikuta akipoteza kibarua chake baada ya hapo jana Chelsea kukubali kipigo cha goli moja kwa nunge wakati ilipocheza na West Bromwich.