Pata taarifa kuu
LIGI KUU YA UINGEREZA

Manchester United yaendelea kuwafukuzia kwa karibu mahasimu wao Man City

Mchezaji wa Man Utd Wyne Rooney akiifungia timu yake bao la kwanza dhidi ya Tottenham
Mchezaji wa Man Utd Wyne Rooney akiifungia timu yake bao la kwanza dhidi ya Tottenham Reuters

Ligi kuu ya nchini Uingereza imeendelea kuwa ngumu na isiyotabirika huku vigogo viwili Manchester United na Manchester City wakiendelea kuchuana kileleni mwa ligi hiyo wakitofautiana kwa alama mbili.

Matangazo ya kibiashara

Hapo jana klabu ya Man utd iliendeleza wimbi lake la ushindi baada ya kufanikiwa kuwafunga timu ngumu ya Totenham Hotspurs ambayo inapewa nafasi kubwa ya kuwemo kwenye zile timu ambazo zinawania nasfai nne za juu.

Katika mchezo huo uliopigwa kwenye dimba la White hart Lane ulishuhudia Man Utd wakichomza na ushindi wa mabao 3-1 na kupunguza tofauti ya alama na mahasimu wao Man city ambapo sasa wanatofautiana kwa alama mbili.

Magoli ya Manchester United yaliwekwa kimiani na mchezaji Wyne Rooney na Ashley Young aliyefunga mabao mawili wakati goli la kufutia machozi la tottenham likiwekwa kimiani na mchezaji aliyeingia kipindi cha pili Defoe.

kwa matokeo hayo Man Utd inafikisha alama 64 nyuma ya vinara wa ligi hiyo Man City yenye alama 66.

Mechi nyingine iliwakutanisha Newcastle Utd ambayo ilikuwa na kibarua dhidi ya Sunderland kwenye mchezo ambao ulishuhudia timu hizo zikitoka sare ya bao moja kwa moja.

Katika mchezo mwingine klabu ya Fulham ilifanikiwa kuchomoza na ushindi mnono wa mabao matano kwa nunge dhidi ya klabu Wolves.

Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.