LIGI YA MABINGWA ULAYA

Barcelona yafanya kufuru yamagoli dhidi ya FC Beyern Liverkusen ligi ya mabingwa Ulaya

Mchezaji wa FC Barcelona Lionel Messi akifunga moja ya bao kati ya magoli matano aliyoifungia timu yake jana kwenye mchezo wa ligi ya mabingwa Ulaya
Mchezaji wa FC Barcelona Lionel Messi akifunga moja ya bao kati ya magoli matano aliyoifungia timu yake jana kwenye mchezo wa ligi ya mabingwa Ulaya Reuters

Timu ya FC Barcelona imeendelea kudhihirisha yenyewe ndio klabu bora ya karne baada ya kufanya kweli kwenye uwanja wake wa nyumbani kwa kuibuka na ushindi wa mabao saba kwa moja.

Matangazo ya kibiashara

Kwenye mchezo huo ambao ulipigwa kwenye dimba la Nou Camp ulishuhudia klabu ya Barcelona ikiwachezesha kwata timu ya Beyern Liverkusen ya Ujerumani kwa kufanikiwa kuchomoza na ushindi wa magoli 7-1.

Shujaa wa mchezo huo alikuwa ni mchezaji bora wa dunian Lionel Messi ambaye peke yake alifanikiwa kufunga mabao matano kati ya saba ambayo yaliiwezesha timu yake hiyo kufuzu hatua ya robo fainali kwa kishindo.

Mabao mwengine mawili ya Barcelona yaliwekwa kimiani na mchezaji Cristian Herrera Tello na kukamilisha idadi ya mabao saba kabla ya wageni Liverkusen hawajapata bao la kufutia machozi kupitia kwa Karim Bellarabi.

Mchezo mwingine ulishuhudia klabu ya APOEL Nicosia na wao wakifanikiwa kufuzu kwenye hatua ya robo fainali baada ya kuibuka na usindi wa penalt nne kwa tatu baada ya kushudia timu hizo zikimaliza dakika tisini zikiwa sare ya bao moja kwa moja.

Kwa matokeo hayo APOEL ilifanikiwa kuibuka na jumla ya mabo matano kwa manne dhidi ya Lyon ya Ufaransa ambayo itajutia mchezo huo kutokana na kukosa magoli mengi ya wazi.