Pata taarifa kuu
UINGEREZA

Hali ya Muamba yaimarika.

football365.com
Ujumbe kutoka: Sabina Chrispine Nabigambo
1 Dakika

Hali ya kiungo wa timu ya Bolton Wanderers Fabrice Muamba imeripotiwa kuwa imara baada ya kuanguka na kupoteza fahamu hapo jana wakati wa mchezo wa robo fainali ya kombe la FA baina ya timu yake na Tottenham.

Matangazo ya kibiashara

Muamba aliripotiwa kupoteza fahamu baada ya kuanguka akiwa peke yake katika dimba la White Hart Lane na kupelekwa katika hospitali ya Chest ya jijini London ambako anapatiwa matibabu chini ya uangalizi maalum.

Kufuatia tukio hilo muda mfupi baadaye mchezo huo ulisitishwa huku timu zote zikiwa zimetoshana nguvu ya bao moja kwa moja.

Taarifa kutoka vyanzo vya hospitali ya Chest zinaeleza kuwa hali ya Muamba inazidi kuimarika.
 

Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.