Pata taarifa kuu
Uingereza

John Terry kukosa mchuano wa Chelsea dhidi ya Manchester City

Dakika 2

Nahodha wa klabu ya soka ya Chelsea nchini Uingereza John Terry atakosa mchuano wa ligi kuu nchini humo  dhidi ya Manchester City katika uwanja wao wa nyumbani wa Etihad Jumatano hii.

Matangazo ya kibiashara

Terry ambaye alirudi uwanjani baada ya kupona jeraha la goti,alijeruhiwa tena wakati wa mchuano wa klabu bingwa barani Ulaya, dhidi ya Napoli na kukosa mchuano wa kombe la FA mwishoni mwa wiki iliyopita dhidi ya Leicester.

Kaimu kocha wa Chelsea Roberto Di Matteo anakiri kuwa mchuano dhidi ya Manchster City utakuwa mgumu kwa vijana wake na atakosa mchango wa Terry ambaye anatarajiwa kupata nafuu kabla ya mchuano wa Jumamosi dhidi ya Tottenham.

Katika michuano mingine ya katikati ya juma,Tottenham watakuwa wenyeji wa Stoke City,Everton watakuwa katika uwanja wao wa nyumbani wa Goodison Park dhidi ya Arsenal,wakati Queens Park Rangers wakiwakaribisha Liverpol.

Manchester United inaongoza msururu wa ligi kuu ya Uingereza kwa alama 70 ikifuatwa na Manchester City kwa alama 66.

Tottenham Hotspurs ni ya tatu kwa alama 53 wakati Arsenal ikifunga nne bora kwa alama 52.

Queens Park Rangers,Wigan na Wolverhampton zinavuta mkia kwa alama 22.
 

Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.