Barcelona

Messi anahitaji bao moja kuweka Historia Barcelona

Lionel Messi anahitaji bao moja pekee kufikia rekodi ya mchezaji wa zamani Cesar Rodriguez aliyeweka rekodi ya mfungaji bora  katika klabu ya Barcelona .

Matangazo ya kibiashara

Historia inaonesha kuwa,Rodriguez alifunga jumla ya mabao 235 wakati akiicheza Barcleona miaka ya hamsini na si 232 kama ilivyokuwa imeelezwa hapo awali.

Hata hivyo,Messi anaweza kufikia rekodi hiyo ikiwa atafunga bao katika mchuano wa Barcelona na Granada FC Jumanne usiku.

Hadi sasa,Messi ameifungia Barcelona zaidi ya magoli 200 tangu alipoanza kuicheza klabu hiyo mwaka 2007,na msimu huu amefunga mabao 51 katika ligi hiyo ya La Liga.

Messi mwenye umri wa miaka 24 raia wa Argertina anajivunia rekodi ya kuwa mchezaji bora duniani mtawalia na msimu huu ameendelea kuonesha ubabe wake katika mchezo wa soka.

Rodriguez wakati akiichezea Barcelona kwa kipindi cha miaka 13 aliongoza katika safu ya ufungaji mabao kwa misimu saba alizocheza.